Besas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Besas (alifariki 19 Machi 251 hivi) alikuwa askari Mkristo huko Aleksandria (Misri).

Akitetea Juliani na Eunus, waliokuwa wanatukanwa na kupigwa kwa imani yao, alipelekwa kwa hakimu na hatimaye, akidumu katika imani hiyo, akakatwa kichwa wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.

Habari zao na za wafiadini wengine kumi zimesimuliwa na barua ya Dionisi wa Aleksandria kwa Fabiani wa Antiokia.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Februari[1] au 30 Oktoba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.