Bendera ya Iceland
Mandhari
Bendera ya Iceland imepatikana tangu mwaka 1915. Ina rangi ya buluu ikionyesha msalaba mweupe ndani yake. Ndani ya msalaba nyeupe kuna msalaba mwembamba zaidi nyekundu.
Muundo wa bendera ni ile ya bendera zote za Skandinavia zinazofuatamfano wa bendera ya kale ya Denmaki inayoitwa Danebrog.
Rangi ya buluu inaikumbusha rangi ya anga juu ya Aisilandi.
Kwa ujumla inafanana mno na bendera ya Unowe isipokuwa kwa kubadilishana rangi. Aisilandi ina uhusiano wa karibu sana na Unowe tangu mwanzo wake.