Bendera ya Uturuki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bendera ya Uturuki iliyo rasmi (kwa Kituruki: Türk bayrağı) ni bendera nyekundu iliyo na nyota nyeupe na mwezi mpevu.

Bendera ya Uturuki mara nyingi huitwa al bayrak (bendera nyekundu), na inaitwa al sancak (bendera nyekundu) katika İstiklal Marşı, wimbo wa taifa wa Uturuki.

Ubunifu wa sasa wa bendera ya Uturuki umetokana moja kwa moja na bendera ya Dola la Osmani, ambayo ilipitishwa mwishoni mwa karne ya 18 na kupata namna yake ya mwisho mnamo 1844. Vipengele vya bendera ya Uturuki vimefafanuliwa na Sheria ya Bendera ya Uturuki mnamo 29 Mei 1936.