Bendera ya Uswidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Uswidi

Bendera ya Uswidi ni ya rangi buluu yenye msalaba njano wa kulala. Muundo wake umefuata muundo wa Danebrog ya Denmark jinsi ilivyo na bendera zote za Skandinavia.

Chaguo la rangi kimetokana na nembo ya mfalme wa Uswidi. Bendera imepatikana tangu mwaka 1663.

Kuna utaratibu wa kuonyesha bendera: hupandishwa kila siku saa 2 asubuhi, kati ya Novemba hadi Februari saa 3 asubuhi (miezi penye giza). Inashushwa wakati wa kuchwa au mwisho saa 3 usiku (katika miezi ya mwanga giza inachelewa au kupotea kabisa).