Basiano na wenzake
Mandhari
Basiano na wenzake ni kundi la Wakristo wa karne ya 3 waliofia dini yao kwa namna mbalimbali huko Aleksandria (Misri).
Kati yao kuna: padri Sirioni, halafu Agatoni na Mose waliochomwa moto, Dionisi na Amoni waliouawa kwa upanga, Tonioni, Proto, na Lusio waliotoswa baharini pamoja na Basiano.
Pengine wanahesabiwa kuwa 26 au 30 na baadhi kutajwa kwa majina haya: Armata, Arbasi, Orus, Paulo, Plesius, Pasamona na Hipus, ambao lakini hawatajwi katika Martyrologium Romanum kwa kuwa labda wanahusika na kundi lingine linaloadhimishwa tarehe 9 Februari[1].
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 14 Februari[2][3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |