Baaziz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Baaziz akiwa kwenye tamasha

Baaziz, jina la sanaa Abdelaziz Bekhti, (alizaliwa 1963 huko Cherchell, kaskazini mwa Algeria ) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Algeria[1].

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Ingawa anaishi Ufaransa, Baaziz ni mmoja wa waimbaji na watunzi wa nyimbo mahiri zaidi wa nchini Algeria. Baaziz alivutia mashabiki kwa wimbo wake wa kwanza wa "ya Hasrah kikount Esseghir" (kwa Kiingereza Once upon a time I was a kid ). Katika muda mwingi wa kazi yake alipigwa marufuku nyimbo zake kuchezwa kwenye redio na TV za Algeria.

Hata hivyo, wimbo wake uliompa mafanikio zaidi ulikua "Algeria My Love," ulimsababisha kutambuliwa maalum kutoka kwa Rais Bouteflika. [2] Na kukubalika na serikali ya Algeria, hata hivyo, kulidumu kwa muda mfupi. Uamuzi wake wa kuimba wimbo wa kuwashutumu majenerali wa Algeria, "Waili Waili," kwenye kipindi cha televisheni cha moja kwa moja licha ya onyo ulisababisha apigwe na kulaumiwa. [3]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2008 Baaziz alitangaza nia yake ya kugombea katika uchaguzi wa urais wa Algeria . [4] Hata hivyo ugombea huo haukutimia na akatangaza kuwa hatamuunga mkono yeyote kati ya wagombea. [5]

Orodha ya kazi zake za muziki[hariri | hariri chanzo]

  • Chaâbi Rock'n Bled (2005)
  • Café de l'independance (2004)
  • Dorénavant (1999)
  • Coyotte
  • Ybip-Emmou
  • El-Rebelle
  • The Best

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Les Enchanteurs ont accueilli Baaziz et sa valise de chansons engagées". web.archive.org. 2011-07-10. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-10. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
  2. "L'indépendence de Baaziz", Radio France Internationale, 28 June 2004. Retrieved on 16 March 2010. 
  3. Martin, Marie-Hélène (2008). Le Petit Futé Algérie. Petit Futé. uk. 131. ISBN 978-2-7469-2196-2. 
  4. "Baaziz candidat à la présidentielle?", Jeune Afrique, 10 December 2008. Retrieved on 16 March 2010. 
  5. "" Je ne soutiens aucun candidat à la présidentielle "", El Watan, 23 March 2009. Retrieved on 16 March 2010.