Azzedine Mihoubi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mihoubi,_Azzedine

Azzedine Mihoubi (Alizaliwa mnamo Januari 1, mwaka 1959), ni mwanasiasa, mshairi,mwanariwaya na pia alikuwa mwandishi wa habari,Azzedine Mihoubi anahudumu kama Waziri wa Tamaduni nchini Algeria.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

‘’’Azzedine Mihoubi’’’alizaliwa mnamo Januari 1, mwaka 1959 huko ‘’’Khadra’’’, Algeria.[1] Alihitimu katika École nationale d'administration d'Alger mnamo mwaka 1984.[1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Mihoubi alianza kazi yake ya uandishi wa habari mnamo 1986.Alikuwa mkuu wa habari kwenye runinga ya Algeria kutoka 1996 hadi 1997.Alifanya kazi kama mtendaji mkuu wa redio ya Algeria kutoka 2006 hadi 2008,na maktaba ya taifa ya Algeria kuanzia 2010 hadi 2013.

Mihoubi alikuwa mjumbe wa Bunge la Wananchi kutoka 1997 hadi 2002.

Mihoubi ni mwandishi wa vitabu kumi ya mashairi na riwaya nne.Pia amepokea zawadi mbalimbali za fasihi kwa ushairi wake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 BIOGRAPHIE : AZZEDINE MIHOUBI. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-10-18. Iliwekwa mnamo December 3, 2016.