Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini-Mashariki
Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini-Mashariki (Association of Southeast Asian Nations - ASEAN) ni ushirikiano wa kimataifa wa nchi za upande wa kusini mashariki wa bara la Asia.
Unaunganisha mataifa 10 yaliyoko kijiografia na kisiasa kati ya nchi kubwa za China na Uhindi. Shabaha yake ni kuboresha ustawi wa uchumi, maendeleo ya kijamii na ya kiutamaduni na kutunza amani ya sehemu hii ya dunia.
Umoja huu ulianzishwa mwaka 1967 na Indonesia, Malaysia, Ufilipino, Singapur na Uthai. Baadaye Brunei, Kambodia, Laos, Myanmar na Vietnam zlijiunga nao.
Tangu kwa na nchi wanachama 10 eneo la umoja huu ulikuwa 4,500,000 [[km2]] na uchumi wake unakua haraka ulifikia pato la trilioni USD $1.4 mnamo mwaka 2008. Jumla ya wakazi ilikuwa watu 575,000,000 ambayo ni sawa na 8% za watu wote duniani.
Takriban theluthi moja ya watu hawa ni Waislamu (milioni 240) walioko hasa Indonesia na Malaysia. Uthai, Myanmar, Laos, Kambodia na Vietnam wako hasa wafuasi wa Ubudha.
Uchumi unastawi hasa kutokana na malighafi kama mafuta ya petroli pamoja na bidhaa za elektroniki. Nchi za Asean zimefaulu kwa ujumla kuondoka kwenye umaskini mkali na kujenga uchumi wa viwandani.
Nchi zote zina tamaduni za kale za kienyeji zilizosimama imara hata wakati wa ukoloni.
Umoja huu una mikutano ya kila mwaka.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- ASEAN Secretariat Archived 26 Agosti 2009 at the Wayback Machine. tovuti rasmi
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
}