Assisi
Assisi | |
Nchi | Italia |
---|---|
Mkoa | Umbria |
Wilaya | Perugia |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 26,946 |
Tovuti: http://www.comune.assisi.pg.it/ |
Assisi (inatamkwa Asizi) ni mji wa Italia, mkoa wa Umbria, wilaya ya Perugia. Wakazi wake ni 26.946 (2007).
Ni maarufu hasa kwa kuwa ndiko alikozaliwa mtakatifu Fransisko (1182-1226), shemasi aliyeanzisha utawa wenye matawi mbalimbali ambao ni mkubwa kuliko mashirika yote ya Kanisa Katoliki.
Miaka hiyohiyo huko walizaliwa pia kaisari Federiko II, Klara wa Asizi na Anyesi wa Asizi.
Baadaye tena hukohuko alizaliwa mtakatifu mwingine, Gabriele wa Mama wa Mateso.
Sehemu mbalimbali za mji huo zimo katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kwa asili Asizi ni mji wa Kirumi ambao ulipata umuhimu kwa sababu unatawala barabara kuu ya mkoa wa Umbria kutoka Spoleto (ambayo katika Karne za Kati ilikuwa makao ya mfalme mdogo aliyekuwa chini ya mfalme mkuu wa Ujerumani) hadi Perugia mji uliokuwa chini ya utawala wa Papa.
Wakati huo kulikuwa na ushindani mkubwa kati ya Asizi uliokuwa chini ya mfalme mkuu na jirani yake Perugia uliosimama upande wa Papa.
Mbali ya hayo ndani ya mji wenyewe yalianza mapigano kati ya mayores (wakubwa, yaani masharifu) na minores (wadogo) yaliyosababisha masharifu wengi kukimbilia Perugia na hivyo kuzidisha chuki kati ya miji hiyo. Matokeo yake ni mapambano ya mwaka 1202 ambayo Fransisko pia aliyashiriki akashikwa mateka kwa mwaka mzima.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiitalia) Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 19 Novemba 2020 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Assisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |