Asmaa Mahfouz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Asmaa Mahfouz kwenye Uwanja wa Tahrir, Kairo

Asmaa Mahfouz (kwa Kiarabu أسماء محفوظ; alizaliwa mwaka 1985) ni mwanaharakati, mwandishi wa blogu na mwanzilishi mmojawapo wa Harakati ya Vijana wa 6 Aprili nchini Misri.

Wito wake kwa blogu kuandamana 25 Januari 2011[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Januari 2011 vijana Wamisri wanne waliwahi kujichoma moto kutokana na kukata tamaa kwa sababu ya hali duni ya nchi na maisha yao. Asmaa alitumia blogu yake ya video kupinga udikteta wa rais Hosni Mubarak na hali duni ya haki za binadamu nchini. Alisema, "Wamisri wanne walijichoma kwa kupinga aibu ya udhalilishaji, njaa na umaskini waliopaswa kuishi nazo kwa miaka 30. ... Leo hii mmoja wao amefariki." Akaendelea kuwaambia wananchi, "tuone aibu fulani ... Badala ya kujichoma moto tufanye kitu cha maana. Kuketi nyumbani na kufuatilia habari tu kwa TV au facebook itatupeleka penye udhalilishaji."[1]

Aliita wananchi kukutana kwenye uwanja wa Tahrir mjini Kairo tarehe 25 Januari 2011. Video yake alipeleka YouTube ilipoangaliwa na wengi. Video hii iliendelea kuwa ishara ya kuanzisha mapinduzi ya Misri ya 2011.

25 Januari kama chanzo cha mapinduzi[hariri | hariri chanzo]

Siku iliyotajwa kwenye blogu malakhi ya Wamisri walifika uwanja wa Tahrir. Polisi 30,000 walishindwa kuwafukuza, mamia walikamatwa, mjini Suez wananchi 2 waliuawa na polisi wakati wa maandamano. Maandamano yalifuatana siku kwa siku hadi kujiuzulu kwa serikali na hatimaye rais Mubarak mwenyewe mnamo Februari 2011.

Kukamatwa kwa Asmaa[hariri | hariri chanzo]

Mwezi Agosti mwaka huohuo Asmaa alikamatwa na kushtakiwa mbele ya mahakama ya kijeshi kwa sababu ya kukosoa Kamati Kuu ya Kijeshi[2] iliyowahi kuchukua nafasi ya rais aliyepinduliwa tayari. Aliachishwa baadaye.[3][4][5][6]

Tuzo la Sakharov[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Oktoba 2011 Asmaa Mahfouz aliteuliwa, pamoja na wanaharakati wengine wa Misri, kwa Tuzo la Sakharov linalotolewa na Bunge la Ulaya kwa sababu alitetea haki za binadamu kwa kuwapa Wamisri motisha ya kudai haki zao kwenye uwanja wa Tahrir kwa njia ya video na blogu zake kupitia Youtube, Facebook na Twitter.[7] Tarehe 14 Desemba 2011 Asmaa alipokea mwenyewe tuzo hili katika sherehe maalumu kwenye bunge la Ulaya huko Strasbourg.[8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. LeVine, Mark (25 January 2012). "Egypt: The revolution that shame built". Aljazeera. Iliwekwa mnamo 14 February 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Freedom Alert: Egyptian activist Asmaa Mahfouz arrested". August 2011. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-23. Iliwekwa mnamo 2017-03-08.  Check date values in: |date= (help)
  3. "Egyptian military drops charges against activists". Financial Times. 
  4. "Egyptian military drops charges against activists". August 2011.  Check date values in: |date= (help)
  5. Egypt blogger Mahfuz quizzed for 'defaming' military BBC News. 14 August 2011
  6. Osman, Ahmed Zaki Activist released from military court on LE20,000 bail for Facebook post Archived 15 Agosti 2011 at the Wayback Machine. Al Masry Al Youm. 14 August 2011
  7. "The Arab Spring wins Sakharov Prize 2011". European Parliament. 27 October 2011. Iliwekwa mnamo 14 February 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  8. "EU parliament honours Asmaa Mahfouz with Sakharov prize". AhramOnline. 14 December 2011. Iliwekwa mnamo 14 February 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: