Apoloni na Filemoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Apoloni na Filemoni (walifariki karibu na Antinoe, 307 hivi) walikuwa Wakristo wa Misri waliofia imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian.

Apoloni alikuwa mmonaki shemasi, kumbe Filemoni alikuwa mwanamuziki aliyemtukana na kumdhihaki. Kwa kuona alivyojibiwa kila mara kwa upole na wema aliongokea Ukristo na kujitambulisha kwa hakimu. Hatimaye waliuawa pamoja.

Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi[1][2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.