Nenda kwa yaliyomo

Apolinari wa Laodikea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Apolinari wa Laodikea (alifariki mwaka 390) alikuwa mwanateolojia aliyefundisha kwamba Yesu hakuwa na akili ya kibinadamu; badala yake alisema Yesu Kristo alikuwa na mwili na upande wa chini tu wa roho (zinapotokea hisia) lakini akili yake ilikuwa ya Kimungu.

Inaonekana alifundisha hivyo katika juhudi za kupinga Uario uliokanusha umungu wa Yesu.[1]

Baada ya kupingwa na Theodoreto wa Kuro na Basili Mkuu, fundisho hilo lililaaniwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 362, iliyoongozwa na Atanasi wa Aleksandria, na hatimaye kutajwa kama uzushi na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381), uliosisitiza kwamba Kristo ni Mungu kamili na mtu kamili.

  1. McGrath, Alister. 1998. Historical Theology, An Introduction to the History of Christian Thought. Oxford: Blackwell Publishers. Chapter 1.
  • Catholic Encyclopedia entry
  • Artemi, E., «Mia physis of God Logos sesarkomeni» a)The analysis of this phrase according to Cyril of Alexandria b)The analysis of this phrase according to Apollinaris of Laodicea»,Ecclesiastic Faros t. ΟΔ (2003), 293 – 304.
  • McGrath, Alister. 1998. Historical Theology, An Introduction to the History of Christian Thought. Oxford: Blackwell Publishers. Chapter 1.
  • Edwards, Mark (2009). Catholicity and Heresy in the Early Church. Ashgate. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.