Alipi wa mnarani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Alipi wa Adrianopoli)
Mchoro mdogo wa Mt. Alipi.

Alipi wa mnarani (kwa Kigiriki: Ἀλύπιος ὁ Στυλίτης, Alyupios o Stylítis; Adrianopoli, Paflagonia, leo nchini Uturuki, 515 hivi - Adrianopoli, 614) alikuwa shemasi ambaye aliishi kama mkaapweke na kupata umaarufu kwa kuishi miaka 40 juu ya mnara[1].

Kutokana na sifa hiyo iliyomvutia wanafunzi wengi, aliweza kuanzisha monasteri mbili, kwa wanaume na kwa wanawake.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Novemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.