Ajantha Perera
Ajantha Wijesinghe Perera ni mwanasayansi, mhadhiri wa chuo kikuu, mwanaharakati wa mazingira na mwanasiasa wa Sri Lanka. [1] Anajulikana kwa juhudi zake za kumaliza mzozo wa takataka nchini Sri Lanka na anajulikana kama Malkia wa Taka. [2] Alianzisha Mpango wa Kitaifa wa Urejelezaji wa Taka Ngumu ili kutatua mzozo wa takataka. [3] [4]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Ajantha Perera alimaliza masomo yake ya juu nchini Uingereza na kurudi Sri Lanka akiwa na umri wa miaka 23. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Kelaniya kama mhadhiri msaidizi wa Biokemia, Fiziolojia na Zoolojia . Alijiunga na Chuo Kikuu cha Colombo kama mhadhiri mkuu katika Mafunzo ya Mazingira ambapo pia alikamilisha kuhitimu kwake. [5]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Perera amefanya kazi kama mtaalam katika wizara kadhaa nchini Sri Lanka na Fiji . Kwa sasa anafanya kazi za kutengeneza mkakati wa usimamizi wa urejeleaji wa taka ngumu nchini. [6] Alipendezwa na siasa mwaka 2019 na kugombea Chama cha Kisoshalisti cha Sri Lanka kwenye Uchaguzi wa Rais wa 2019 na alipata kura 27,572 akidai nafasi ya saba kati ya wagombea. [7] [8]
Alikua mgombea Urais wa kwanza mwanamke kugombea katika uchaguzi baada ya miaka 20. [9] [10]
Mnamo Februari 2020, alijiunga na chama cha UNP kufuatia mwaliko uliopendekezwa na kiongozi wa UNP Ranil Wickremesinghe na kusisitiza kwamba babu yake pia alikuwa amewakilisha chama icho hapo awali. [11] Alishiriki pia katika uchaguzi wa 2020 wa ubunge wa Sri Lanka akiwakilisha Chama cha Kitaifa cha Umoja kutoka wilaya ya Colombo. [12] [13]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Dr. Ajantha Perera pledges a corruption-free nation | Daily FT". www.ft.lk (kwa English). Iliwekwa mnamo 2019-10-01.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Socialism is about giving power to the working class - Dr Ajantha Perera". Sunday Observer (kwa Kiingereza). 2019-10-12. Iliwekwa mnamo 2019-10-14.
- ↑ "Focus on having more women in politics, says Dr. Perera | Daily FT". www.ft.lk (kwa English). Iliwekwa mnamo 2019-11-18.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Presidential candidates throw in their hats for the top job". Times Online - Daily Online Edition of The Sunday Times Sri Lanka. Iliwekwa mnamo 2019-10-14.
- ↑ "Plus". www.sundaytimes.lk. Iliwekwa mnamo 2019-10-01.
- ↑ "Ajantha Perera". Ashoka | Everyone a Changemaker (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-10-01.
- ↑ "ජනාධිපතිවරණයට ඉදිරිපත්වන කාන්තාව".
- ↑ "Presidential Election - 2019: Final Result - All Island". Retrieved on 2022-05-31. Archived from the original on 2019-11-17.
- ↑ "ජනාධිපතිවරණයට ඉදිරිපත්වන කාන්තාව".
- ↑ "Women and politics | Daily FT". www.ft.lk (kwa English). Iliwekwa mnamo 2019-10-01.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Ajantha Perera: Former Presidential candidate joins UNP". CeylonToday (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-12.
- ↑ "The UNP is a party with a history - Dr. Ajantha Perera". www.dailymirror.lk (kwa English). Iliwekwa mnamo 2020-08-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Dr. Ajantha joins UNP to contest General Election from Colombo". Sri Lanka News - Newsfirst (kwa Kiingereza). 2020-02-28. Iliwekwa mnamo 2020-08-12.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ajantha Perera kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |