Nenda kwa yaliyomo

Adolfo na Yohane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Adolfo na Yohane (Sevilia, Hispania - Cordoba, Hispania, 824) walikuwa watoto wa baba Mwislamu na mama Mkristo waliouawa na mtawala wa eneo hilo, Abd-ar-Rahman II kwa kuongokea na kukiri hadharani imani ya Kikristo na hivyo kuhesabiwa na ndugu wa baba na serikali kama waasi.

Baadaye dada yao, Aurea, akiguswa na mfano wao, aliwafuata katika dini na katika kuifia[1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 27 Septemba[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Jessica Coope: Martyrs of Cordoba: Community and Family Conflict in an Age of Mass Conversion: Lincoln: University of Nebraska Press: 1995: ISBN 0-8032-1471-5.
  • Kenneth Wolf: Christian Martyrs in Muslim Spain: Cambridge: Cambridge University Press: 1988: ISBN 0-521-34416-6.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.