Wakristadelfiani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Christadelphian Hall, Bath, England

Wakristadelfiani (kutoka jina la Kiingereza "Christadelphians") ni dhehebu dogo la Kikristo lililoanzishwa katika Uingereza na Marekani wakati wa karne ya 19. Jina lilibuniwa na mwanzilishaji wake John Thomas aliyeunganisha maneno ya Kigiriki "khristos" (Kristo) na "adelfoi" (ndugu" kwa maana " ndugu wa Kikristo".

Kwa hiyo maana ya jina Kristadelfiani ni 'Ndugu katika Kristo'.[1] Wapo duniani kote kadri ya wanachama 55~65,000 pamoja.[2]

Yaliyomo

[hariri] Imani

Wakristadelfiano wanadai ya kwamba wanaamini mafundisho yote ya Biblia ambayo ni pamoja na:[3]

  • 1. Biblia ndio ujumbe pekee na wa kweli kutoka kwa Mungu na ilipeanwa kwa ujumia na Yeye.
  • 2. Kuna Mungu mmoja pekee, Baba, aliyeumba dunia na anakusudi kubwa nayo.
  • 3. Roho Mtakatifu ni uwezo (nguvu) wa Mungu mwenyewe, ambayo uitumia kufanya mapenzi yake matakatifu.[4]
  • 4. Yesu ni mwana wa Mungu. Yeye pia ni mwana wa Adamu kupitia kuzaliwa kwake na Mariamu.[5]
  • 5. Yesu alishinda majaribu yote na akafa awaokoe wafuasi wake kutoka kwa dhambi na mauti.
  • 6. Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu na Mungu. Baadaye alipaa mbinguni lakini atarudi.
  • 7. Wakati ararudi atawafufua na kuwahukumu waumini waliokufa na kuwapa kutokufa (uzima wa milele) wale waaminiifu.
  • 8. Atakuwa mfalme juu ya ufalme wa Mungu utakaoru-dishwa Israeli, na juu ya dunia nzima.[6]
  • 9. Wafuasi wake ambao watakuwa na miili hisiyoweza kufa watamsaidia kuleta haki ya milele na amani duniani kote.
  • 10. Ibilisi sio kiumbe kisicho cha ulimwengu huu yaani si malaika lakini ni jina lengime la dhambi, iharibiwayo tu katika Kristo.[7][8][9]
  • 11. Wokovu unausiana na kufunikwa kwa dhambi kupitia kwa Yesu na uhuru kutoka kwa dhambi na mauti wakati atakaporudi.
  • 12. Wakati mtu anapokufa ukoma kuishi. Tumaini pekee ya uhai ni ufufuo wakati Yesu atarudi.
  • 13. Kuamini katika ahadi za Mungu juu ya ufalme wake na kazi za Yesu Kristo ni muhimu.[10]
  • 14. Toba na ubatizo katika Kristo kwa kuzikwa ndani ya maji na ufuasi wa kila siku wa Kristo ni muhimu kwa wakovu hatimaye.[11]

[hariri] Jamii

[hariri] Utaratibu wa Iklezia (kanisa)

Watumishi wa Iklezia, yaani (1) Mwenyekiti, (2) Katibu, (3) Mtunza Hazina na (4) Mkaguzi wa Hesabu. Iklezia mpya watahitaji ndugu wanne ili kutenda kazi wakiwa ni watumishi wa Iklezia na kushika kazi mahususi. Watumishi wa Iklezia hawatakiwi kutawala iklezia, bali watende kazi kama watumishi wa Bwana na wa ndugu zao na dada. Hawatakiwi wao wawe madikiteta katika mambo ya Iklezia bali kama watumishi wa Bwana na wa Iklezia. Hawatakiwi kuishi kwa pesa za Iklezia au kujiona wenyewe ni wachungaji au watu wa kuheshimiwa sana kama Padri n.k.[12]

[hariri] Marejeo

  1. Wakristadelfiani Nani? CBM Tanzania
  2. The Columbia Encyclopedia, Sixth Edition, 2009
  3. Tennant, Harry. The Christadelphians, what they believe and teach. CMPA Birmingham 1987
  4. Tennant H. Biblia Yaonyesha Kuwa ni Uwezo wa Mungu (The Holy Spirit) CMPA
  5. Hayward A. Ni kweli Yesu Kristo alishuka kutoka mbinguni? (Did Jesus really come down from heaven?) CBM 1979
  6. Fred Pearce Unabii wa Biblia Bible Prophecy
  7. Mshitaki wen Iblisi CBM
  8. Ulukilanio Lwa Mündu (The Serpent) CBM Tanzania
  9. Malaika: Wajumbe wa Mungu (Angels: God's Messengers) CMPA
  10. David M. Pearce Fungu Lako Katika Ahadi za Mungu (Your Share in Gods Promises) CMPA
  11. Matayarisho ya Ubatizo (Preparing for Baptism) CBM
  12. Kuanzisha Iklezia ya Kristadelfiani (CBM) (Starting a Christadelphian Ecclesia) CBM Tanzania

[hariri] Viungo vya nje

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine