Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispania
Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispania ilipiganiwa kati ya 1936 na 1939 kati ya watetezi wa serikali ya jamhuri ya Hispania na wafuasi wa kiongozi wa kijeshi jenerali Francisco Franco. Franco alishinda akawa kiongozi na dikteta wa Hispania hadi kifo chake mwaka 1975.
Yaliyomo |
Utangulizi wa vita [hariri]
Siasa ya Hispania ilikuwa katika hali ya vurugu tangu kuanzishwa kwa jamhuri ya pili mwaka 1931 iliyomaliza utawala wa mfalme Alfonso XIII. Sehemu kubwa za wafanyakazi wa viwandani hazikuridhika na jamhuri wakalenga kwa mapinduzi ya kijamii. Harakati kali ya upinzani dhidi ya nafasi kubwa ya kanisa katoliki kwenye taifa la Hispania ilisababisha mashambulio shidi ya makanisa na monasteri na vifo vya watu.
Wafuasi wa mfalme aliyeondoka nchini, watetezi wa kanisa katoliki, wenye mashamba makubwa na chama kipya cha Falange walianza kujiunga katika upinzani kwa jamhuri na katiba yake kwa ujumla.
Baada ya majaribio ya vikosi vya wafanyakazi wasoshalisti lakini pia wanajeshi wapenzi wa mfalme waliolenga wote kupindua serikali uchaguzi wa 1936 haukuleta usuluhisho wa matata ya siasa. Vikundi viwili vikubwa vilivyoshindana vilikuwa "umoja wa wananchi" uliouinganisha wasoshalisti, wakomunisti na vikundi vodogo dhidi ya "umoja wa taifa" uliounganisha wafuasi wa mfalme, wakatoliki, chama cha wenye mashamba na Falange. Umoja wa wananchi ulipata kura chache zaidi kuliko wapinzani wake na sheria ya uchaguzi uliupa nafasi nyingi bungeni.
Franco kutwaa silaha [hariri]
Vurugu iliendelea na baada ya mauaji ya kisasa sehemu za jeshi chini ya jenerali Franco zilichukua silaha dhidi ya serikali ya jamhuri. Sehemu kubwa ya jeshi ilijiunga naye.
Serikali ya jamhuri ilikuwa na sehemu nyingine ya jeshi lakini viongozi wanegi walikuwa upande wa upinzani. Kila upande ulitolea silaha kwa wanamigambo walioundwa na vyama mbalimbali vya kisiasa.
Watetezi wa jamhuri walipata usaidizi kutoka serikali za Umoja wa Kisovyeti na Meksiko na wapinzani walisaidiwa na serikali za Benito Mussolini nchini Italia na Adolf Hitler nchini Ujerumani. Marafiki wa jamhuri ya Hispania walikuja kutoka nchi nyingi na kushika silaha wakaitwa vikosi vya kimataifa ("international brigades").
Guernica kama mfano wa ukali wa vita [hariri]
Mapigano yalikuwa makali na watu wengi waliuawa hovyo. Mwishowe jeshi la Franco ilishinda akisaidiwa na vikosi vya jeshi la Italia na Ujerumani.
Kati ya mapigano mengi lilitokea shambulio la ndege za kijeshi za Kijerumani dhidi ya mji wa Guernica iliyokuwa kati ya mashambulio ya kwanza ya idadi kubwa ya ndege dhidi ya mji duniani. Guernica iliharibiwa na Pabo Picasso alichora taswira iliyokuwa maarufu.
Hispania ya Franco [hariri]
Baada ya ushindi wa Franco 1939 vyama vya upande wa jamhuri vilipigwa marufuku na vyama vyote vya upinzani vililazimishwa kuungana katika Falange chini ya uongozi wa Franco mwenyewe.