Mangosuthu Buthelezi
Inkosi Mangosuthu ("Gatsha") Ashpenaz Nathan Buthelezi (amezaliwa tar. 27 Agosti 1928) ni kiongozi wa Kizulu huko nchini Afrika Kusini, na vile vile kiongozi wa chama cha Inkatha Freedom Party (IFP) ambacho kiliundwa mwaka 1975.
Yaliyomo |
Wasifu [hariri]
Maisha ya awali [hariri]
Mangosuthu alizaliwa mnamo tar. 27 Agosti mwaka wa 1928, mjini Mahlabathini, KwaZulu-Natal, na Chief Mathole Buthelezi na binti wa mfalme Magogo kaDinizulu, ambaye ni dada wa mfalme Solomon kaDinuzulu. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Impumalanga iliyoko Mahashini, Nongoma, tangu mwaka 1933 hadi mwaka 1943, kisha katika chuo kimoja kiitwacho Adams College, kilichopo Amanzimtoti, tangu mwaka 1944 hadi 1947.
Baadae akaelekea katika Chuo Kikuu cha Fort Hare kuanzia mwaka 1948 hadi 1950, ambapo huko ndiko aliko jiunga na chama cha African National Congress Youth League na kuanza kupata mawasiliano na Robert Mugabe na Robert Sobukwe. Mangosuthu alifukuzwa Chuoni baada ya wanafunzi kuleta mgomo. Kisha baadae alikuja kumalizia Digrii yake katika Chuo Kikuu cha Natal.
Marejeo [hariri]
- William Beinart, "Twentieth Century South Africa", Oxford, 2001, pg. 330
Viungo vya nje [hariri]
- Wasifu kuhusu Buthelezi
- Habari zinazo jadili kuhusu kupigwa chini kwa Buthelezi kuwa kama Waziri mkuu wa mambo ya ndani
- Chief Mangosuthu Gatsha Buthelezi
- Asili ya kabila la Buthelezi
- [1]
- [2]
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mangosuthu Buthelezi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |