Gairo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kata ya Gairo
Nchi Tanzania
Mkoa Morogoro
Wilaya Kilosa
Idadi ya wakazi
 - 35,638


Gairo ni jina la makao makuu ya Wilaya ya Gairo katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2002, kata ya Gairo ilikuwa na wakazi wapatao 35,638, wengi wao wakiwa Wakaguru. [1]

Gairo ni mojawapo ya miji ambayo inakua sana nchini na unajulikana kwa kuwa unazalisha mazao ya biashara na chakula kama vile viazi vitamu, mahindi, maharagwe na vilevile kwa ufugaji.

Kutokana na ukaribu wake na barabara kuu ya Dodoma, mji wa Gairo umekuwa moja ya walishaji wakubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Hapo zamani Gairo ilikuwa chini ya jimbo la uchaguzi la Kilosa, baadaye ulipata kuwa jimbo linalojitegemea. Mnamo Machi 2012 umefanywa wilaya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Repoti Kuu ya Hesabu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2002 (en). Serikali ya Tanzania. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-03-20.
Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Gairo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.