Iyogwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Iyogwe ni kata ya Wilaya ya Gairo katika Mkoa wa Morogoro , Tanzania, yenye Postikodi namba 67708.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 9,744 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 23,286 waishio humo.[2]

Wakazi walio wengi ni wa kabila la Wakagulu na wachache ni Wanguu. Wakagulu walio wengi ni waumini wa dini ya kikristo na Wanguu walio wengi ni waumini wa dini ya kiislamu.

Jina la Iyogwe lilitokana na mabishano ya Wakagulu wawili kuhusu njia: mwingine akisema "iyogweye" akiwa na maana 'hiyohiyo njia' lakini mwenzake alikuwa hakubaliani naye, hapo ndipo jina la Iyogwe lilipopatikana mpaka leo.

Iyogwe ni kijiji ambacho kina sifa katika Wilaya ya Gairo kwa ujumla, hasa katika ulinzi na usalama wa jadi ujulikanao kama Uwu ama Umwano wa Ukaguru.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2015-03-22.
Kata za Wilaya ya Gairo - Mkoa wa Morogoro - Tanzania

Chagongwe | Chakwale | Chanjale | Chigela | Gairo | Idibo | Italagwe | Iyogwe | Kibedya | Leshata | Madege | Magoweko | Mandege | Mkalama | Msingisi | Nongwe | Rubeho | Ukwamani


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iyogwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.