Eustorji wa Milano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eustorji wa Milano

Mchoro wa ukutani katika basilika lake huko Milano.
Feast

Eustorji wa Milano (alifariki 350 hivi) alikuwa Askofu wa 9 wa mji huo, Italia Kaskazini katikati ya karne ya 4[1].

Inasemekana alitokea Ugiriki akawa gavana wa Milano hadi alipochaguliwa kuwa askofu.

Atanasi wa Aleksandria alimsifu kwa kulinda imani sahihi dhidi ya Waario na Ambrosi alimsifu kama askofu aliyeteseka kwa ajili ya imani hiyo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Septemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.