Elsie Garrett Rice

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Elsie Garrett Rice (Cape Town, 25 Novemba 1869 - 27 Aprili 1959[1]) alikuwa Mwingereza na msanii wa sanaa za uchoraji wa mimea aliyezaliwa nchini Afrika Kusini.

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Wazazi wa Elsie Garret Rice walikuwa Mary Gray na Reverend John Feydell Garrett.[2]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Elsie na pacha wake John Herbert Garrett walibatizwa tarehe 16 Januari 1870.Elsie pamoja na ndugu zake watatu John,Edmund na Amy walikuwa Yatima ambao walilelewa na binamu yao Millicent Fawcett na Agnes Garrett. Millicent alikuwa mwanachama hai katika harakati za Suffragist Movement na aliolewa na Henry Fawcett.

Alisoma katika shule ya sanaa ya Slade School of Art.

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Rice alikuwa mkufunzi katika shule ya Bedales School, ambayo ilianzishwa na shemeji yake John Haden Badley mnamo mwaka 1865 hadi mwaka 1967. akiwa katika shule hiyo ndipo alipokutana na mume wake Charles Emmanuel Rice mwaka 1865 hadi mwaka1949, Mwalimu mkuu wa King Alfred School alikuwa Hampstead.Mnamo mwaka 1901 Rice alikuwa akiishi na mume wake na mtoto mmoja wa kiume na mmoja wa kike hadi kufikia mwaka 1911, Elsie alikuwa ni mwalimu wa sanaa mwenye umri wa miaka 41 aliekuwa akiishi Steep, Hampshire pamoja na mume wake mwenye umri wa miaka 45 pamoja na watoto wao wawili Gabriel Edmund mwenye umri wa miaka 11 na Agnes Rosemary mwenye umri wa miaka 10, na wote walizaliwa Hampstead.Mwaka 1918 Charles Rice alihitimu masomo yake ya udaktari .[3]

Elsie alitengana na mume wake na kwenda kuishi Afrika Kusini mwaka 1933, ambapo aliishi Rondebosch na kisha kuhamia Camps Bay pamoja na binti yake Rosemary Agnes.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 'Botanical Exploration of Southern Africa' - Gunn & Codd (Balkema, 1981)
  2. "Elsie Garrett Rice Biography | Annex Galleries Fine Prints". www.annexgalleries.com. Iliwekwa mnamo 2021-01-31. 
  3. Heesom, D. (March 1, 1977). "A distinguished but little known artist: Elsie Garrett-Rice". Veld & Flora 63 (1): 23 – kutoka journals.co.za.  Check date values in: |date= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elsie Garrett Rice kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.