Bundi (Tytonidae)
| Bundi | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Bundi (pia mabundi) ni ndege mbua wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Ukurasa huu unahusu familia Tytonidae. Spishi hizi zina rangi ya kahawa nyuma na nyeupe mbele zenye madoa madogo meusi. Kichwa chao kina umbo wa mviringo na uso mwao una umbo wa moyo. Bundi hula ndege na wanyama wadogo, wanyama wagugunaji hasa, lakini wadudu wakubwa pia. Jike huyataga mayai 2-7 kwa mahali palipofunika kama tago lililoachwa na ndege mwingine ndani ya tundu ya mti, ufa wa mwamba, dari la nyumba au kihenge n.k.
Bundi huwinda usiku na hupumzika mchana. Walilenga windo lao kwa msaada ya masikio yao. Manyoya ya uso yapeleka mawimbi ya sauti kwa vipenyo vya masikio viliopo mahali tofauti kidogo kimoja kuliko kingine. Hivyo waweza kulikamata windo bila kuliona. Windo hawezi kumsikia bundi akija, kwa sababu mabawa ya bundi hayafanyi sauti yo yote kwa kuwa kingo ya mbele ya manyoya ya mabawa imekerezekakerezeka na ile ya nyuma ina matamvua. Hii yapunguza vurugu ya hewa na kwa hivyo uvumi.
Yaliyomo |
Spishi za Afrika [hariri]
- Phodilus prigoginei, Bundi wa Kongo (Congo Bay Owl)
- Tyto alba, Bundi Babawatoto (Western Barn Owl)
- Tyto capensis, Bundi-mbuga (African Grass Owl)
- Tyto soumagnei, Bundi Mwekundu (Red Owl)
Spishi za mabara mengine [hariri]
- Phodilus assimilis (Sri Lanka Bay Owl)
- Phodilus badius (Oriental Bay Owl)
- Tyto aurantia (Golden Masked Owl)
- Tyto delicatula (Eastern Barn Owl)
- Tyto deroepstorffi (Andaman Masked Owl)
- Tyto glaucops (Ashy-faced Owl)
- Tyto inexspectata (Minahassa Masked Owl)
- Tyto longimembris (Eastern Grass Owl)
- Tyto manusi (Manus Masked Owl)
- Tyto multipunctata (Lesser Sooty Owl)
- Tyto nigrobrunnea (Taliabu Masked Owl)
- Tyto novaehollandiae (Australian Masked Owl)
- Tyto novaehollandiae troughtoni (Cave-nesting Masked Owl) – udhabiti si hakika, yamkini imekwisha (miaka 1960)
- Tyto rosenbergii (Sulawesi Owl au Sulawesi Masked Owl)
- Tyto rosenbergii pelengensis (Peleng Masked Owl) - yamkini imekwisha (kati ya karne ya 20)
- Tyto sororcula (Moluccan Masked Owl)
- Tyto (sororcula) cayelii (Buru Masked Owl) – labda imekwisha (kati ya karne ya 20?)
- Tyto tenebricosa (Greater Sooty Owl)
Spishi za kabla ya historia [hariri]
- Tyto cf. alba/aurantiaca (New Ireland Lesser Barn Owl)
- Tyto balearica (mwisho wa Miocene – kati ya Pleistocene ya Mediteranea)
- Tyto cavatica (Puerto Rican Barn Owl) – labda iliishi bado mwaka wa 1912; labda spishi ndogo ya T. glaucops
- Tyto jinniushanensis (Pleistocene ya Jing Niu Shan, China)
- ?Tyto letocarti (New Caledonian Barn Owl)
- Tyto melitensis (Maltese Barn Owl) – zamani katika jenasi Strix, labda spishi ndogo ya Tyto alba
- Tyto mourerchauvireae (kati ya Pleistocene ya Sisilia, Mediteranea)
- Tyto noeli (Noel's Barn Owl, Kuba)
- Tyto cf. novaehollandiae (Mussau Barn Owl)
- Tyto cf. novaehollandiae (New Ireland Greater Barn Owl)
- Tyto ostologa (Hispaniolan Barn Owl)
- Tyto pollens (Bahaman Barn Owl) – labda iliishi mpaka karne ya 16
- Tyto riveroi (Rivero's Barn Owl, Kuba)
- Tyto robusta (mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene ya Rasi ya Gargano, Italia)
- Tyto (robusta) gigantea (mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene ya Rasi ya Gargano, Italia)
- Tyto sanctialbani (kati – mwisho wa Miocene ya Ulaya wa Kati) – zamani katika jenasi ya Strix
- Tyto sp. (Cuban Barn Owl)
- Tyto sp. (Barbuda Barn Owls, Barbuda na yamkini Antigua) – angalau spishi 2