Apolinari wa Ravenna
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Apolinari wa Ravenna, mzaliwa wa Antiokia, (Syria ya kale, leo Antakya, nchini Uturuki) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo wa Italia hadi alipouawa huko kwa ajili ya imani yake.) Kwa hiyo anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Julai.