Zoë Wicomb

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Zoë Wicomb
Alizaliwa 23 Novemba 1948
Nchi Afrika Kusini
Kazi yake mwandishi na mtaalamu wa fasihi

Zoë Wicomb (alizaliwa 23 Novemba 1948) ni mwandishi na mtaalamu wa fasihi nchini Afrika Kusini-Scottish ambaye ameishi nchini Uingereza tangu mwaka 1970.[1] Mwaka 2013 alitunukiwa tuzo ya Nobel kwa kazi yake ya fasihi.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Zoë Wicomb alizaliwa karibu na Vanrhynsdorp, Rasi ya Magharibi, nchini Afrika Kusini. Alikulia katika mji mdogo wa Namaqualand, alikwenda Cape Town kusoma shule ya sekondari, na alisoma Chuo Kikuu cha Western Cape (ambacho kilianzishwa mwaka 1960 kama chuo kikuu cha "Coloreds").[2][3]

Baada ya kuhitimu, alihama Afrika Kusini mwaka wa 1970 na kwenda Uingereza, ambako aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Reading. Aliishi huko Nottingham na Glasgow na kurudi Afrika Kusini mwaka 1990, ambapo alifundisha kwa miaka mitatu katika idara ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Western Cape.

Mwaka 1994, alihamia Glasgow, Uskoti, ambapo alikuwa Profesa wa Uandishi na Ubunifu katika Chuo Kikuu cha Strathclyde hadi kustaafu kwake mwaka 2009. Alikuwa Profesa katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch tangu mwaka wa 2005 hadi 2011. Pia ni profesa mstaafu wa chuo kikuu cha Strathclyde.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Neel Mukherjee, "Homing instinct: October by Zoë Wicomb", New Statesman, 26 June 2014.
  2. "UWC History", University of the Western Cape.
  3. "Zoe Wicomb A Writer Of Rare Brilliance". Interview by David Robinson for The Scotsman, 2000; via Intermix.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zoë Wicomb kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.