Zakaria Kibona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zakaria Kibona
Maelezo binafsi
Jina kamili Zakaria Kibona
Tarehe ya kuzaliwa 14 Machi 1990 (1990-03-14) (umri 34)
Mahala pa kuzaliwa    Dar es salaam, Tanzania
Urefu Sentmita 180
Nafasi anayochezea Mshambuliaji
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Atlantis FC
Namba 14
Klabu za vijana
Atlantis FC
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2008 Atlantis FC
Timu ya taifa
2000-2004
2004-
2006-
Tanzania U-15
Tanzania U-17
Tanzania

* Magoli alioshinda

Zakaria Kibona (alizaliwa 14 Machi 1990, jijini Dar es Salaam) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Tanzania, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Atlantis FC inayoshiriki katika ligi ya pili ya Ufini katika mji mkuu wa Helsinki nchini Ufini.

Kuanza kwake mpira Ufini[hariri | hariri chanzo]

Zakaria ni mshambuliaji matata wa kati ambaye alijiunga na Atlantis FC ya vijana mwaka 2002 na alicheza na klabu hiyo hadi mwaka 2007 baada ya kocha wa klabu ya Atlantis FC ya watu wakubwa kuomba apandishwe katika timu ya wakubwa na baadae alionekana kuwa ni mchezaji mzuri ambae kwa sasa anacheza mechi nyingi nakuwa kiungo muhimu wa timu hiyo.

Timu ya Taifa ya Tanzania[hariri | hariri chanzo]

Bwana Zakaria Kibona aliichezea timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wa umri mdogo ya miaka 15 na miaka 17 kabla ya mwaka 2006 kuitwa kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania ya watu wakubwa na kwa sasa anamechi 15 na timu ya Taifa hiyo ya Tanzania.

Uraia wake[hariri | hariri chanzo]

Zakariba Kibona ana uraia wa nchi ya Tanzania na Ufini na alipata uraia wa Ufini kwani mchezaji huyo alienda Ulaya akiwa na umri mdogo nakukaa huko muda mrefu, na sio yeye tu ambae alichukua uraia katika wachezaji mpira kuna wachezaji mashuhuri ambao walichukua uraia kutokana na maslahi yao fulani kama kulipa ushuru au mengine na baadhi yao ni kama vile Ronaldinho, Samuel Eto'o na wengine pia.

Zawadi[hariri | hariri chanzo]

Kuchukua ubingwa pindi alipokua akichezea Atlantis FC ya vijana mwaka 2006 katika mashindano ya vijana.

Viongo vya nje[hariri | hariri chanzo]