Zaituni Njovu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zaituni Njovu
Zaituni Njovu akiwa na tuzo ya Mtetezi bora wa haki za binadamu,2019

Zaituni Njovu ni mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali liitwalo Zaina Foundation lililoanzishwa mwaka 2017. Makao makuu ya shirika hilo yapo Dar es Salaam. Lengo kuu la kuanzishwa shirika hili ni kuwawezesha wanawake katika teknolojia haswa kupitia warsha na mafunzo mbalimbali ya elimu ya kidijitali na kutafsiri programu mbalimbali za teknolojia kwa lugha ya Kiswahili. Zaituni Njovu ni mhamasishaji wa matumizi ya intaneti nchini Tanzania[1] [2]

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Zaituni alizaliwa mkoani Tanga lakini asili yake ni Mkoa wa Ruvuma. Alipata elimu ya msingi mkoa wa Tanga na baadae alifaulu hadi kufika Chuo Kikuu cha Arusha ambapo alisoma ualimu wa kufundisha kompyuta. Zaituni ni mpenzi wa kusoma teknolojia, kusafiri na kukutana na marafiki wapya, mara nyingi akitumia teknolojia kuwakutanisha watu na kujenga urafiki.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2018 Zaituni alishinda tuzo ya Mtetezi Bora wa Haki za Binadamu barani Afrika tuzo ambayo ilitolewa na shirika la kimataifa la Kutetea haki za binadamu katika wakati wa kidijitali liitwalo Access Now [3]

Njovu alipatiwa tuzo hiyo ya heshima Tunisi Juni 2019 wakati wa Rightcon Tunis 2019 , kutokana na kazi yake ya kuwasaidia wanawake kuweza kutumia teknolojia kwa lugha ya Kiswahili ambapo Zaina Foundation imekuwa ikitafsiri programu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumiwa na wanawake wa Tanzania na Afrika Mashariki.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zaituni Njovu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.