Yustini na Atilano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yustini na Atilano (majina kamili kwa Kihispania Justino Orona Madrigal, aliyezaliwa tarehe 14 Aprili 1877, na Atilano Cruz Alvarado, aliyezaliwa tarehe 5 Oktoba 1901; waliuawa Rancho de las Cruces, Guadalajara, Mexico, 1 Julai 1928) walikuwa mapadri wa Kanisa Katoliki nchini Meksiko hadi walipouawa bila kesi wakati wa Vita vya Wakristero[1].

Yustini aliwahi kuanzisha shirika la Masista Waklara wa Moyo Mtakatifu[2].

Papa Yohane Paulo II aliwatangaza wenye heri tarehe 22 Novemba 1992 halafu watakatifu wafiadini tarehe 21 Mei 2000 pamoja na wenzao 24 waliofia dini katika vita hivyo[3]:

Sikukuu ya wote pamoja inaadhimishwa kila tarehe 21 Mei ila ya kwao wenyewe ni tarehe ya kifodini chao[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.