Nenda kwa yaliyomo

Yemi Alade

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yemi Alade
Yemi Alade
[[Image:Amezaliwa=Machi 13,1989|220px|]]
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Yemi Eberechi Alade
Asili yake Abia, Nigeria
Aina ya muziki Afro pop
Miaka ya kazi 2005-hadi sasa

Yemi Eberechi Alade (kwa kifupi hujulikana kama Yemi Alade; amezaliwa 19 Machi 1989) ni mwimbaji kutoka nchini Nigeria akifanya muziki wa Afropop na pia ni mwandishi wa nyimbo mbalimbali. Mwanamuziki huyu amekuwa akifahamika kutokana na kibao chake kijulikanacho kama Johnny.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Yemi alade alizaliwa Abia, nchini Nigeria akiwa ni mtoto wa James Alade na Helen Uzoma. Baba yake alikua kamanda wa Jeshi la polisi mwenye asili ya kiyoruba na mama yake alikua pia kamanda wa jeshi la polisi mwenye asili ya Igbo. Yemi Alade ni mtoto wa tano katika familia yenye watoto saba. Elimu yake ya msingi alisoma katika shule iitwayo St. Savior British Primary School na baadae kusoma elimu yake ya sekondari katika shule iliyoitwa Victory Grammar School huko jijini Lagos na baadae alisomea Jiografia katika Chuo kikuu cha Lagos.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
Kichwa Yaliyomo
King of Queens
Mama Africa
  • Ilitolewa: Machi 25, 2016
  • Lebo: Effyzzie Music Group
  • Aina: Digital download, CD
Black magic
  • Ilitolewa: Disemba 15, 2017
  • Lebo: Effyzzie Music Group
  • Aina: Digital download, CD
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yemi Alade kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.