Nenda kwa yaliyomo

Wilaya ya Mbinga Vijijini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Mbinga (kijani) katika mkoa wa Ruvuma.

Wilaya ya Mbinga ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Ruvuma yenye postikodi namba 57400.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 353,683 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 285,582 [2] baada ya maeneo yake kadhaa kutengwa kuwa wilaya ya Nyasa mwaka 2012 na mji wa Mbinga kuwa halmashauri ya pekee mwaka 2015.

Wilaya hii imepakana na mkoa wa Iringa upande wa kaskazini, wilaya za Songea mjini na Songea vijijini upande wa mashariki, Msumbiji upande wa kusini na Ziwa Nyassa upande wa magharibi.

Sehemu kubwa ya eneo lake iko ndani ya milima inayoongozana na pwani ya ziwa pamoja na mwambao wa ziwa.

Wilaya imeona maendeleo kadhaa kutokana na barabara mpya na kilimo cha kahawa inayostawi vizuri katika hali ya hewa mlimani.

Mji wa Mbinga ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Mbinga.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Living space Mbinga (tovuti ya kikatoliki) Ilihifadhiwa 7 Februari 2017 kwenye Wayback Machine.

Kata za Wilaya ya Mbinga - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania

Amani Makoro | Kambarage | Kigonsera | Kihangi Mahuka | Kipapa | Kipololo | Kitumbalomo | Kitura | Langiro | Linda | Litembo | Litumbandyosi | Lukarasi | Maguu | Mapera | Matiri | Mbuji | Mhongozi | Mikalanga | Mkako | Mkumbi | Mpapa | Muungano | Namswea | Ngima | Nyoni | Ruanda | Ukata | Wukiro


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mbinga Vijijini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.