Mapera (Mbinga)
Kwa matunda yenye jina hili angalia makala kuhusu Pera
Kata ya Mapera | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Ruvuma |
Wilaya | Mbinga |
Mapera ni jina la kata ya Wilaya ya Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania yenye postikodi namba 57432 .[1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,513 waishio humo.[2]
Mapera ni kata mpya iliyoanzishwa mwaka 2010 baada ya kuigawa kata ya Maguu. Kabla ya kupandishwa hadhi na kuwa kata Mapera ilikuwa ni kijiji kimojawapo cha kata ya Maguu.
Kata ya Mapera inaundwa na vijiji vya Mkinga , Kihongo, Lukanzauti na Mapera yenyewe ambayo ni makao makuu ya kata.
Wakazi wa Mapera ni wa kabila la Wamatengo.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Kata za Wilaya ya Mbinga - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Amani Makolo | Kambarage | Kigonsera | Kihangi Mahuka | Kipapa | Kipololo | Kitumbalomo | Kitura | Langiro | Linda | Litembo | Litumbandyosi | Lukurasi | Maguu | Mapera | Matiri | Mbuji | Mhongozi | Mikalanga | Mkako | Mpapa (Mbinga) | Muungano | Namswea | Ngima | Nyoni | Ruanda (Mbinga) | Ukata | Wukiro |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mapera (Mbinga) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |