Linda
Kata ya Linda | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Ruvuma |
Wilaya | Mbinga |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 13,371 |
Linda ni kata ya Wilaya ya Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania yenye postikodi namba 57414.
Kata hiyo ina jumla ya vijiji sita ambavyo ni Ulolela, Liyombo, Linda, Silo, Ndembo na Mkaranga.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 13,371 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,111 waishio humo.[2]
Wakazi wa kata hiyo ni Wamatengo na asilimia kubwa ya watu hao ni wakulima. Kilimo chao kikuu cha biashara ni kahawa. Aidha chakula chao kikuu ni ugali na maharagwe.
Kata hiyo ina jumla ya zahanati tatu zinazotoa huduma ya afya na jumla ya shule nane ambazo zinatoa elimu. Aidha kati ya hivyo, sita zinatoa elimu ya shule ya msingi na viwili vinatoa elimu ya sekondari.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Mbinga - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania | ||
---|---|---|
Amani Makoro | Kambarage | Kigonsera | Kihangi Mahuka | Kipapa | Kipololo | Kitumbalomo | Kitura | Langiro | Linda | Litembo | Litumbandyosi | Lukarasi | Maguu | Mapera | Matiri | Mbuji | Mhongozi | Mikalanga | Mkako | Mkumbi | Mpapa | Muungano | Namswea | Ngima | Nyoni | Ruanda | Ukata | Wukiro |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Linda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |