Nenda kwa yaliyomo

Wanawake wa Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wanawake wa Tanzania wanazidi kupata nafasi katika maisha ya jamii, kama ilivyothibitishwa na uwepo wa rais Samia Suluhu Hassan. Vilevile mwaka 2022 wanashika asilimia 36 ya wabunge wote, na kwa mara ya pili Bunge limepata Spika mwanamke, tena kuna mawaziri tisa na wakuu wa mikoa wanne wanawake[1]. Kwa upande mwingine, kati ya wenyeviti wa vijiji 11,915, asilimia 2.1 tu ni wanawake, kati ya wenyeviti wa mitaa 4,171, asilimia 12.6 tu ni wanawake na kati ya wenyeviti wa vitongoji 62,612 ni asilimia 6.7 tu ambao ni wanawake; tena kwa wabunge, kati ya wale wa majimbo 238, asilimia 9.1 tu ndiyo wanawake[2].

Pia usalama wa wanawake nchini Tanzania umeimarika kwa kiasi kikubwa tangu karne ya 20, hata hivyo taifa linasalia kuwa jamii yenye mfumo dume ambapo wanawake wanakabiliwa na viwango vya juu vya ukatili wa kijinsia [3][4]