Nenda kwa yaliyomo

Umani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wamani)

Umani (au Umanikeo, kutoka jina la Kiingereza "Manicheism") ni dini iliyoanzishwa na Mani (216-274 hivi) huko Mesopotamia, wakati ilikuwa sehemu ya milki ya Uajemi katika karne ya 3 BK.

Mani alibuni dini yake kwa kusudi akilenga kuunganisha Uzoroasta, Ukristo na Ubuddha. Alitazama ulimwengu kuwa na nguvu mbili ambazo ni mwanga na giza, sawa na mema na mabaya. Dini hiyo ilifuata ujuzilio na kuenea sana katika Uajemi, upande wa magharibi katika Dola la Roma na upande wa mashariki hadi China.

Kati ya watu walioisadiki, maarufu zaidi ni Augustino wa Hippo, aliyoifuata kwa miaka kadhaa kabla hajaongokea Ukristo wa Kanisa Katoliki na kutunga maandiko dhidi ya Umani.

Katika karne zilizofuata, jina la "Umani" lilitumiwa na waandishi Wakristo dhidi ya mafundisho mbalimbali yaliyotazamiwa kama uzushi na kuonyesha tabia za uwili, hata kama hazikutokana na Umani wa kihistoria.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Tafsiri za Kiingereza kwa vyanzo vya Kimani[hariri | hariri chanzo]

Maandiko juu ya Umani[hariri | hariri chanzo]