Wafiadini wa Nitria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wafiadini wa Nitria (waliofariki karne ya 4) ni kati ya Wakristo bora wa Misri waliofia dini yao kwa kuuawa na wazushi.

Walikuwa wamonaki wanne na askofu wa Aleksandria ambao Yohane Krisostomo aliandika juu yao.

Hayajulikani mengine kuhusu historia yao, hata majina, ila tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 10 Julai[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.