Nenda kwa yaliyomo

Vurugu vya kina (Vitisho)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vurugu kina hurejelea onyesho la vitendo dhahiri, katili na halisi vya vurugu katika uwasilishaji, kama vile filamu, televisheni, na michezo video . Huenda ikawa halisi, uigizaji wa uhailsia, au iliyohuishwa .

Kwa kusudi ya kutazamwa na hadhira komaa, hali ya uwazi, pasi na haya huzingatiwa.

Vipengele

[hariri | hariri chanzo]

Maneno yafuatayo huhusishwa na vurugu vya kina.

Ufafanuzi wa udamu ni taswira inayoonyesha damu au jeraha la kuogofya. [1] [2] Kwenye mtandao, neno hili hutumika kama ujumla wa picha zote halisi ya kudhulumiwa kwa mwili, kama vile ukeketaji, ajali za kazini na ukatili kwa wanyama . Wakati mwingine neno "udamu tibabu" hutumiwa kurejelea picha halisi za upasuaji.

Neno hili mara nyingi huchukuliwa kuwa kisawe cha "vurugu vya kina", lakini baadhi ya watu au mashirika hutofautisha kati ya maneno haya. Mfano mmoja ni Adobe Inc., ambayo hutenganisha maneno haya kwa huduma yake ya uchapishaji. [3] Mfano mwingine ni tovuti habari maalum The Verge . Inatenganisha maneno haya wakati wa kuripoti kufungwa kwa LiveLeak, tovuti ambayo ilitumiwa kupangisha video za kutisha kabla ya kufungwa. [4]

Kueneza video za kidamu ni kinyume cha sheria. [5]

Udhalimu wa watoto

[hariri | hariri chanzo]

Udhalimu huu huhusisha ponografia kithiri ya watoto, unaowadhalilisha, kuwaathiri kimwili na kuwaua kwa mbinu inayohusisha unyanyasaji wa kingono kwa watoto . [6] [7] [8] [9]

Picha za kina na filamu halisia

[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya filamu halisia au picha halisi ni za kutisha. Mifano ni kama katika vita na uhalifu. [10] [11] Tofauti na udamu, kushiriki taswira na kanda halisia ni halali, ingawa uchapishaji na uenezi wa picha hizi husababisha mijadala na malalamiko. [12] [13]

Mfano wa mchoro unaowasilisha udamu

Vitisho hujumuisha taswira zozote ya waziwazi kama vile mauaji, matumizi ya silaha, kifo kutokana na ajali au majeraha mabaya, kujiua na udhalimu . Ktika hali zote, ni uwazi huu unaosababisha vurugu hii iwe ya kina. Katika taswira buni, njama tofauti hujumuishwa ili kuongeza hisia za uhalisia (yaani damu leba , silaha bandia, picha bandika ). Ili kuhitimu jina la "vitisho", vurugu inayoonyeshwa lazima kwa ujumla iwe ya asili isiyopunguzwa au isiyozuiliwa; mfano ni kama video ya mtu kupigwa risasi, damu kutoka jeraha, na kuanguka ghafla kutoka kwa jengo.

Vitishu huamsha hisia kali, ikiwemo msisimko, uchefu na hata pengine hofu, kulingana na mtazamaji mwenyewe na mbinu ya maonyesho. Kiwango fulani cha vurugu imechukuliwa kuwa lazima katika filamu za kivita, hasa kwa watu wazima. Huwasilishwa kwa kiasi na namna iliyojadiliwa kwa makini ili kusisimua hisia za watu lengwa bila kuibua karaha au uchefu. Vitendo kithiri, na vya kutisha (hasa yanayohusu ukeketaji ) aghalabu hutumiwa katika matisho ili kuibua hisia kali zaidi za mshtuko (ambazo huenda watazamaji husika walitarajia).

Mada hii ni yenye utata mkuu, kwa kuwa wengi wanaamini kwamba kufichuliwa kwa vurugu hivi husababisha kupoza hisia zinazopinga utendaji wa udhalimu, na kusababisha udhibiti katika picha zinazoenezwa. Kesi moja mashuhuri ilikuwa kuundwa kwa Bodi ya Ukadiriaji wa Burudani wa Marekani mwaka wa 1994. Mataifa mengi sasa huhitaji viwango tofauti vya uidhinishaji kabla ya kazi kutolewa kwa umma.

Hata hivyo, wapinzani huadai kwamba kutazama vurugu hivi kunaweza kuleta utakaso, na "kuwapa mbinu ya kusafisha hisia zinazokinzana na jamii". [14]

Filamu ya Saw hujlikana sana kwa maonyesho yake kina ya vurugu na udamu.

Vitisho hutumiwa mara kwa mara katika matisho, na filamu zinazohusisha uhalifu. Filamu nyingine kama hizi zimepigwa marufuku kutoka nchi fulani kwa maudhui yao makali. Filamu damu hukithiri matisho kwani mateso na mauaji huwa ya kweli.

Mada hii imejadiliwa kutoka zamani, hivi majuzi utafiti uliowasilishwa katika kongamano la kimwaka la Chuo cha Madaktari wa Watoto Marekani ilionyesha kwamba " majabari " katika filamu shujaa kwa wastani walitenda vurugu zaidi kuliko waadui, na hivyo huenda wakatuma ujumbe hasi kwa watazamaji wachanga. [15]

  1. "Definition of GORE". www.merriam-webster.com (kwa Kiingereza). 2024-01-14. Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  2. "Gore Definition & Meaning | Britannica Dictionary". www.britannica.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  3. "Harmful Content: Violence and Gore". www.adobe.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  4. Vincent, James (2021-05-07). "LiveLeak, the internet's font of gore and violence, has shut down". The Verge (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  5. "Edmonton gore website owner sentenced for posting Magnotta video | Globalnews.ca". Global News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  6. Daly, Max (19 Februari 2018). "Inside the Repulsive World of 'Hurtcore', the Worst Crimes Imaginable". Vice. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Desemba 2019. Iliwekwa mnamo 5 Februari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Lux captured: The simple error that brought down the world's worst hurtcore paedophile". 
  8. "GCHQ helped catch 'hurtcore' paedophile, Matthew Falder". 
  9. "5 Things I Learned Infiltrating Deep Web Child Molesters". 
  10. Struck, Julia (2024-01-26). "GRAPHIC WARNING: Ukraine Releases Intense Close Combat Footage, Special Forces Take Out Russian Observation Post". Get the Latest Ukraine News Today - KyivPost (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  11. Vasquez, Lucio (2024-01-26). "Leaked videos appear to show excessive violence, abuse in the Harris County Jail". Houston Public Media (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  12. "Raw videos of violent incidents in Texas rekindle debate about graphic images". (en-US) 
  13. "Why Violent News Images Matter". TIME (kwa Kiingereza). 2014-09-02. Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
  14. Bruder, Margaret Ervin (1998). "Aestheticizing Violence, or How To Do Things with Style". Film Studies, Indiana University, Bloomington IN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-09-08. Iliwekwa mnamo 2007-06-08.
  15. "Good Guys More Violent than Bad Ones in Superhero Films: Study". The News Tribe. Novemba 3, 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-04. Iliwekwa mnamo 2018-11-03.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)