Nenda kwa yaliyomo

Vuga (Tanga)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vuga ni kata ya Wilaya ya Bumbuli katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 11,410 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,128 waishio humo.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tangu kuja kwa Mbegha, Vuga ilikuwa mji mkuu wa wafalme wa Washambaa kwa kipindi cha karne ya 18 na 19[2]. Mnamo 1850 ilikuwa na wakazi 3,000 ambayo ni idadi kubwa katika kipindi kile. Wakati wa kuongezeka kwa biashara katikati ya karne ya 19 mahali pa Vuga mlimani palijionyesha kama hasara kwa sababu machifu wa bondeni walitajirika haraka zaidi. Baada ya kifo cha mtemi Kimweri ye Nyumbai mwaka 1862 Semboja wa Mazinde alipata kipaumbele na Vuga haikuwa tena makao ya kifalme ikarudi kuwa kijiji tu.

Kata za Wilaya ya Bumbuli - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Baga | Bumbuli | Dule "B" | Funta | Kisiwani | Kwemkomole | Mahezangulu | Mamba | Mayo | Mbuzii | Mgwashi | Milingano | Mponde | Nkongoi | Soni | Tamota | Usambara | Vuga


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vuga (Tanga) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.