Vienna Fingers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Vienna Fingers ni aina ya biskuti zilizotayarishwa na kampuni ya Keebler, sehemu ya Kellog's. Biskuti hizi huwa zimetayarishwa kwa njia ya safu tatu hasa mbili za nje zalizo ngumu na aina ya siagi ya ladha ya vanila katikati ya hizo mbili za nje. Zikiwa zinafanana sana na kuki za Oreo, biskuti hizi zimechorwa na kuandikwa jina la bidhaa lakini umbo lake ni tofauti hasa kama kidole. Huwa zimepakiwa katika pakiti nyekundu zenye zimeandikwa majina "Vienna Fingers" na rangi nyeupe.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Vienna Fingers ilikuwa mojawapo ya bidhaa zilizouzwa na kampuni ya Sunshine Biscuits. Kuki hizi ziliuzwa kwanza na Sunshine Biscuits katika mwaka wa 1915 na kuwekwa alama maalum kuwa ni biskuti za Sunshine mnamo Novemba 1947. Umaarufu wa biskuti za Vienna Fingers ulitiwa katika kumbukumbu na mtunga hadithi Neil Simon katika mchezo wa kuigiza wa 1965,The Odd Couple - iliundwa kama filamu ya kuchekesha ya 1968. Katika mchezo huo wa kuigiza, Oscar Madison anajaribu kumvutia Felix Ungar,aliyekuwa amehuzunika, na vitafunio:"Je,utakula biskuti za vanilla? Au Vienna Fingers? Nina kila kitu. [7]

Mnamo Januari 1985, bidhaa hii ilibadilishwa jina. Katika mkutano wa Taasisi ya Masoko ya Vyakula ya 1994, kuki za aina ya za Hydrox na pia zilizoboreshwa za Vienna Fingers zilitangazwa upya na Sunshine Biscuits.

Picha ya karibu ya biskuti ya Vienna Fingers ikionyesha jina lilioandikwa kwa biskuti hiyo

Mwishoni mwa Agosti katika mwaka wa 1994, Sunshine Biscuits ilichangia kikosi cha wanajeshi wa Marekani kutoka Kituo cha Jeshi cha Fort Eustis zaidi ya Vienna Fingers na kuki za Hydrox 21,000. Kampuni hii ilifanya hivi kufuatia shehena kama hiyo ilyotumiwa kwa wanajeshi katika Vita ya Gulf War na maandishi ya mwanajeshi mmoja kwenye pakiti ya Oreo,"Tafadhali tuma kuki". Katika maneno ya kampuni:" mchango wa kuki zinazopendwa zitawapa wanajeshi ladha ya nyumbani na kufanya muda ambao wako mbali na familia kupendeza kidogo ". Vienna Fingers na kuki za Hydrox zilisafirishwa pamoja na wanajeshi hadi kwenye mpaka wa Rwanda na Zaire uliojaa wakimbizi.

Keebler iliponunua Sunshine Biscuits, iliendeleza biskuti za Vienna Fingers kama bidhaa zake. Wakati wa kununuliwa naKeebler, Vienna Fingers zilikuwa zikileta mauzo ya thamani ya $milioni 50. Baada ya kununuliwa na Keebler,toleo jipya la aina ya ladha ya machungwa machungu la kuki hizo lilitolewa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ ["Della Femina Adds Sunshine" http://query.nytimes.com/gst/fullpage.html?res=9505EED71239F93AA15754C0A964948260.]. New York Times: pp. D13. 29 Julai 1982.
  2. ^ See the U.S. Trademark for Vienna Fingers Sandwich
  3. ^ Simon, Neil (1966).The Odd Couple: A Comedy in Three Acts. Samuel French Inc.. pp. 30. ISBN 0573613311.
  4. ^ The Odd Couple: A Comedy in Three Acts,kiliandikwa na Neil Simon. Kilichapishwa Random House, 1966,
  5. ^ See the U.S. Trademark for Vienna Fingers.
  6. ^ Gubbins, Teresa (18 Mei 1994). "Food and games at the supermarket show". The Dallas Morning News: pp. 2F.
  7. ^ a b c Piore, Adam (16 Septemba 1994). "Please Deploy Cookies - Sunshine Sends Them To Soldiers". The Record (Bergen County): pp. D1.
  8. ^ a b “Hail the hollow tree,”Gazeti la Prepared Foods , Machi 1999

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]