Oscar Madison
Oscar Madison ni mhusika katika kipindi cha The Odd Couple kilichoanza kama maigizo ya Broadway, kisha ikawa filamu kisha kipindi cha televisheni.
Katika kipindi cha Odd Couple, Oscar Madison (ikiigizwa na Walter Matthau katika maigizo na, pia, filamu na Jack Klugman katika vipindi vya televisheni) ni mtu wa kufanya mambo mengi, na ni mwandishi wa habari katika gazeti la New York Herald. Yeye huwa goigoi sana lakini ana uhusiano wa nguvu na wa kiajabu na rafiki yake Felix Ungar. Hulka zao tofauti zikiunganishwa na wao kuishi pamoja zilileta vichekesho vingi sana. Katika filamu na vipindi vya televisheni, Oscar alikuwa na uzoefu wa kuvaa kofia ya timu ya New York Mets. Walikuwa tofauti sana,Oscar na Felix, Oscar alikuwa ndiye aliyependa kuzungumza na watu na wanawake ilhali Felix hakuwa na uzoefu katika uhusiano na wanawake.
Kati ya miaka 1982-1983, stesheni ya ABC iliwasilisha kipindi cha ,The New Odd Couple,kikiwa toleo jipya la The Odd Couple.Katika The New Odd Couple,wahusika ni Waamerika wa asili ya Kiafrika wanaoigiza kama Oscar na Felix. Oscar ,katika toleo hili jipya , iliigizwa na Desmond Wilson. Katika toleo hili, Oscar alivaa kofia ya timu ya New York Yankees .
Katika mwaka wa 1985, wanawake wawili waliigiza wahusika wakuu katika maigizo ya The Odd Couple ya Broadway. Rafiki wa Oscar ,mwanamke,alikuwa Olive Madison, iliigizwa na Rita Moreno.
Mwaka wa 1993, Klugman aliigiza jukumu la Oscar katika filamu ya The Od Couple:Together Again akiwa na mwigizaji mwenzake Tony Randall. Klugman aliugua kansa ya koo na akapata shida ya kuzungumza, hii ilihusishwa katika filamu.
Katika toleo la Broadway la maigizo ya The Odd Couple,Nathan Lane aliigiza jukumu la Oscar.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tony and Me, A Story of Friendship. By Jack Klugman Ilihifadhiwa 17 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- Jack Klugman's Blog Ilihifadhiwa 26 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.