Frosted Flakes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Frosted Flakes
Ilianzishwa: Katika mwaka wa 1952
Kampuni inayotayarisha: Kellog's

Frosted Flakes ni aina ya chakula cha kiamsha kinywa iliyoanzishwa na Kampuni ya Kellog's. Inahusisha magamba ya mahindi yaliyofunikwa kwa sukari. Jina la "Frosted Flakes" linatumika na kampuni ya Kellog's katika nchi ya Marekani na Kanada. Aina hii ilianzishwa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1952 kama Sugar Frosted Flakes. Neno "sugar" lilitolewa kutoka jina la bidhaa hii katika miaka ya 1980 katika wakati ambao bidhaa nyingi za aina hii zilitoa neno hilo kutoka majina yao.

"Frosted Flakes", kwa jina lenyewe, linaeleza aina ya bidhaa hii. Hivyo basi, jina hili haliwezi kuwa jina linalotumika na kampuni moja tu na linaweza kutumika na kampuni yoyote inayotayarisha bidhaa sawa kama hii. Ingawaje, "Kellog's Frosted Flakes" na "Frosties" ni majina maalum yaliyosajiliwa na kampuni kisheria katika masoko yao maalum.

Majina ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Bidhaa husika za Kellog's Frosties[hariri | hariri chanzo]

 • Katika mwaka wa 2003, Kellogg's ilianzisha Tony's Cinnamon Krunchers. Kaulimbiu ya bidhaa hii ilikuwa "They're Great 'till They're Gone." Bidhaa hii iliachwa kutayarishwa katika mwaka wa 2007 kwa sababu ya mauzo madogo sana.
 • Katika mwaka wa 2004, Kellogg's ilianzisha aina ya chakula hii iliyokuwa na thuluthi ya sukari iliyokuwa katika bidhaa ya hapo awali (yaani bidhaa ya Kellog's Frosted Flakes).
 • Katika mwaka wa 2008, Kellogg's ilianzisha Frosted Flakes Gold. Hii ilikuwa na mionjo ya asali na ilidai kumpa mtu nishati nyingi zaidi kuliko Frosted Flakes ya kawaida.
 • Katika mwaka wa 2009, Kellogg's ilianzisha Frosted Flakes Pink.

Sekta ya Masoko[hariri | hariri chanzo]

Katuni zinazowasilisha bidhaa[hariri | hariri chanzo]

Pakiti ya hapo awali ya Frosted Flakes inayo picha ya katuni ya Tony Tiger

Katuni ya Tony Tiger ndiyo imekuwa ikiwakilisha Frosted Flakes tangu kuanzishwa kwake. Tony anajulikana zaidi kwa kutamka kaulimbiu ya bidhaa hii: "They are Gr-r-reat!". Sauti ya Tony Tiger katika matangazo ya Marekani ilikuwa sauti ya Thurl Ravenscroft mpaka kifo chake katika mwaka wa 2005. Hivi sasa,sauti ya sasa ya katuni hii katika Marekani ni ya Lee Marshall, aliyekuwa mtangazaji. Lee alikuwa amefanya kazi hiyo,ya kuigiza sauti ya Tony, katika tangazo moja la 1997. Anaonekana akiwa amevaa nguo nyekundu kwenye pakiti zote za bidhaa hii. Nchini Uingereza, sauti ya Tony ilifanywa na Thurl Ravenscroft hadi kifo chake kisha Tom Hill akaendelea na kazi hiyo.

Katuni nyingine, Katy Kangaroo, ilichapishwa kwenye pakiti ya Frosted Flakes kwa muda mfupi.

Sentensi maarufu zilizotumika katika uuzaji[hariri | hariri chanzo]

Bidhaa hii imetumia sentensi nyingi katika matangazo yake, lakini iliyotumika sana ni "They're Gr-r-reat!".

 • They're more than good, They're grrrrrrrrreat
 • They're gonna taste great
 • Bring out the tiger in you

! Miaka ya 1980[hariri | hariri chanzo]

 • The taste adults have grown to love. (1980 - 1990)
 • Earn your stripes
 • Never let the tiger catch you
 • Put a tiger on your team
 • Pass it on
 • Scientifically proven better than branflakes and other cereals

Udhamini[hariri | hariri chanzo]

 • Kellogg's alikuwa mfadhili mkubwa wa kipindi cha televisheni cha Adventures of Superman katika miaka mingi ya 1950. Matangazo mengi ya Frosted Flakes yalihusisha mwigizaji wa kipindi hicho , George Reeves. Hivi sasa, matangazo haya yanapatikana katika DVD ya msimu wa kwanza wa kipindi hicho.

Frosties Kid[hariri | hariri chanzo]

Frosties Kid ilikuwa tangazo kwenye mtandao hasa katika mwaka wa 2006. Tangazo hili lilitayarishwa kutoka matangazo yaliyokuwa kwenye stesheni za Uingereza na Ireland yaliyohusisha mvulana akisema "They're gonna taste great".

Fununu kwenye mtandao wa tarakilishi ilikuwa mwigizaji huyo alikuwa amejiua. Fununu hii ilifanya tovuti ya snopes.com kuanza kuchunguza ukweli wa hadithi hii. Katika mwezi wa Juni 2006, ilitangazwa katika stesheni ya BBC Radio One kuwa Frosties Kid alikuwa hai na anaishi nchini Afrika Kusini.

Maswali kuhusu maslahi ya Frosties Kid huulizwa bado na fununu unaovutia watu wengi ni kuwa Frosties Kid alikuwa katuni iliyoumbwa na kampuni ya CGI Creation.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. ^ "Frosties Kid Suicide". Snopes. .
 2. ^ "Frosties CGI: Fact or Fiction". Archived 5 Machi 2010 at the Wayback Machine.
.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]