Froot Loops

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kiwango cha Kuandaliwa: Kikombe Kimoja(36 gramu)
Nishati: 100 kcal
Nishati katika mafuta: 10 kcal
Mafuta yote kwa Jumla: 1 g
Kabohaidreti: 28 g
Nyuzi: 0.6 g
Sukari: 15g
Protini: 1g
Maelezo
Viwango hivi vinaweza kuwa tofauti katika maeneo nje ya soko la Marekani

Froot Loops ni aina ya chakula cha kiamshakinywa kinachotayarishwa na kampuni ya Kellogg's na huuzwa katika nchi zifuatazo: India, Australia, Kanada, New Zealand, Marekani, Ujerumani, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kilatini. Chakula hiki huwa katika vipande vidogo vyenye umbo wa mviringo (hasa lile jina la "loops") na huwa katika rangi mbalimbali na mionjo mbalimbali ya matunda.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kellog's ilianzisha bidhaa za Froot Loops katika mwaka wa 1963. Hapo mwanzoni, kulikuwa na miviringo nyekundu,rangi ya machungwa na manjano,ya kijani kibichi iliongezwa baadaye , kisha zambarau na hatimaye ya samawati ikaongezwa pia.

Aina nyingine ya chakula hii inajulikana kama Froot Loops 1/3 Less Sugar, Marshmallow Froot Loops, na Froot Loops Smoothie.

Katuni ya kuwakilisha bidhaa hii katika matangazo ya televisheni ama kampeni ya bidhaa hii ni Toucan Sam.

Aina Mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Kellogg's imejaribu kupanua bidhaa ya aina ya Froot Loops kwa njia nyingi kwa mfano kwa kuunda Snack Ums. Snack Ums ilikuwa kama nafaka za kawaida za kuliwa kama kiamsha kinywa lakini kubwa zaidi. Kaulimbiu yao ilikuwa "Super sized bites with deliciously intense natural fruit flavors......Flavor bursting! ". Ikimaanisha kuwa ukila chakula hiki chenye mionjo mingi ya matunda, utahisi utamu sana!

Aina nyingine ya Froot Loops iliyoanzishwa na kampuni ya Kellog's ilikuwa Froot Loops Cereal Bar. Froot Loops Cereal Bar ilikuwa nafaka zilizoshikanishwa kwa vyakula vingine mbalimbali katikati ,juu na chini. Hata hivyo, bidhaa hii haikuwa na mafanikio huku maoni mengi ya watu kuwa haikuonja kama nafaka hata kidogo. Kaulimbiu yao ilikuwa "The goodness of cereal and milk!" hasa wakimaanisha "Uzuri wa nafaka na maziwa".

Utamaduni wa Pop[hariri | hariri chanzo]

Froot Loops imehusishwa mara kadhaa katika kipindi cha televisheni cha All in the Family kama nafaka iliyopendwa sana na mhusika Archie Bunker.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ taquitos.net: Snack Ums Froot Loops
  2. ^ taquitos.net: Froot Loops Cereal & Milk Bars

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]