Valeriani wa Cimiez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Valeriani katika kanisa kuu la Nice.

Valeriani wa Cimiez (kwa Kilatini: Valerianus Cemeliensis; alifariki 460 hivi) alikuwa Askofu wa Cimiez (leo mtaa wa Nice, Ufaransa) walau miaka 439 - 455.

Aliwapa waumini na wamonaki mifano ya watakatifu waifuate[1], tunavyoona katika hotuba zake zilizotufikia (Patrologia Latina, 52, c. 691-756)[2].

Hapo awali alikuwa mmonaki huko Lerins.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Julai[3][4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Jean-Pierre Weiss, « Valérien de Cimiez », dans Ralph Schor (coll.), Anthologie des écrivains du comté de Nice, Nice, Serre Éditeur, 1990, p. 13 ISBN 9782864101406.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.