Mto Vaal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vaal (mto))
Mto Vaal

Mto Vaal ni tawimto mrefu wa mto Oranje katika Afrika Kusini.

Chanzo chake ni katika milima ya Drakensberg mkoani Mpumalanga mashariki kwa mji wa Johannesburg.

Inaelekea kusini-magharibi hadi kuungana na mto Oranje karibu na mji wa Kimberley mkoani Northern Cape.

Urefu wake ni km 1120.

Jina la mto limetoka katika lugha ya Kiholanzi; walowezi wa kwanza Waholanzi walitaka kukumbuka mto Waal wa nyumbani kwao.

Vaal ni mto muhimu kwa ajili ya kilimo, viwanda na matumizi ya nyumbani eneo la Johannesburg.

Katika historia ya Afrika Kusini mto Vaal ulikuwa mpaka kati ya koloni la Uingereza kusini kwa mto na jamhuri za Makaburu kaskazini kwa mto. Jina la kihistoria "Transvaal" limemaanisha "ng'ambo ya mto Vaal".

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Vaal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.