Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed
06°34′38″N 003°19′16″E / 6.57722°N 3.32111°E
Kigezo:Infobox airport
Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Murtala Muhammed (Murtala Muhammed International Airport kwa lugha ya kimombo) uko katika sehemu ya Ikeja, nchi ya Lagos, nchini Nigeria, na uwanja huu wa ndege ndio ambao unahudumia mji [1]wa Lagos, kusini magharibi mwa Nigeria na taifa zima. Awali uwanja huu wa ndege ulikuwa unajulikana kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos (Lagos International Airport kwa Kiingereza), lakini jina lake lilibadilishwa ujenzi ulipofikia katikati kuwa Murtala Muhammed ambaye alikuwa mkuu wa zamani wa kijeshi wa Nigeria. Taminalii ya kimataifa ilijengwa kama ya Uwanja wa ndege wa Schiphol iliyoko mjini Amsterdam. Uwanja huu wa ndege ulifunguliwa rasmi tarehe 15 Machi 1979. Uwanja huu ndio wigo kuu kwa ndege kama vile flag carrier airlines ya Nigeria , Nigeria Eagle Airlines na Arik Air.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed ina taminali ya kimataifa na ya taifa (domestic), ambazo zimetenganishwa na umbali wa kilomita moja. Taminali zote zinatumia barabara moja pamoja Taminali ya Taifa ilihamishwa na kupelekwa katiak Taminali ya taifa ya kitambo Lagos mwaka wa 2000 baada ya moto. Taminali mpya ya Taifa ilijengwa na na kupitishwa na tume mnamo 7 Aprili 2007.
Mwaka 2008, uwanja huu wa ndege uliwahudumia abiria 5,136,697.
Historia na sifa
[hariri | hariri chanzo]Katika mwishoni mwa miaka ya 1980 na ya 1990, taminali ya kimataifa ilikuwa na sifa mbaya ya kuwa uwanja wa ndege ambao ni hatari. Kutoka mwaka wa 1992 hadi mwaka wa 2000, US Federal Aviation Administration ilivionya viwanja vya kimataifa vya ndege vya Marekani kwa kuwashauri abiria kwamba hali ya usalama katika LOS haikufikisha yaliyokuwa yanahitajika na ICAO. Mwaka 1993 FAA ilipiga marufukuhuduma za ndege kati ya Lagos na Marekani. Katika kipindi hicho, usalama katika LOS uliendelea kuwa tatizo kubwa. Abiria waliokuwa wakiwasili mjini Lagos walikuwa wanasumbuliwa ndani na nje ya uwanja wa ndege na wahalifu. Wafanyakazi wa uwanja wa ndege walichangia sifa yake. Maafisa wa uhamiaji waliitisha rushwa kabla ya kupiga chapa pasi, na wakati huo huo mawakala wa forodha walidai malipo ya ada ambayo hayakuwepo. Aidha, aina ya ndege ya jet kadhaa zilishambuliwa na wahalifu ambao walikuwa wanasimamisha ndege zilizokuwa zinawasafirisha abiria kutoka na kwenda kwa taminali kisha kuiba mizigo yao. Waongozi wasafiri walipendekeza kuwa abiria wa Nigeria wapitie Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Mallam Aminu Kano katika eneo la Kano na kuchukua ndege za ndani au kusafiri kutumia barabara hadi Lagos.
Kufuatia uchaguzi wa kidemokrasia wa Olusegun Obasanjo mwaka wa 1999, hali ya usalama katika LOS ilianza kuboreka. Polisi wa uwanja wa ndege waliweka sera la " shoot on sight "ambayo inamaanisha kupiga mhalifu kutumia risasi iwapo mtu yeyote atakaye patikana katika maeneo ya usalama kuzunguka barabara ya ndege na sehemu za teksi. Polisi walilinda ndani ya taminali na maeneo ya kuwasili ya nje. FAA iliondoa marufuku ya huduma ya moja kwa moja kwenda Nigeria mwaka wa 2001 katika utambuzi wa maboresho haya ya usalama.
Miaka ya hivi karibuni tumeona marekebisho katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed. Miundombinu zisizofanya kazi na zisizoendeshwa kama vile viyoyozi na vifaa vya kubeba mizigo ya abiria vimerekebishwa. Uwanja nzima wa ndege umesafishwa, mikahawa na maduka yamefunguliwa. Makubaliano ya huduma za anga kati ya Nigeria na nchi nyinginezo vinafufuliwa na vipya vinatiwa saini. Makubaliano haya yameonyesha hisia na haki za kutua kutoka kwa Emirates, Ocean Air Delta na China Southern Airlines katika uwanja wa ndege wa kimataifa kubwa zaidi nchini Nigeria.
Serikali ya Shirikisho imewapa kibali kwa ajili ya upanuzi wa ukumbi wa kuondoka na kuwasili wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed ili kupunguza trafiki inayozidi katika uwanja huo wa ndege.
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Takwimu ya Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed | ||||
mwaka | Jumla ya Abiria | Asilimia ya ongezeko | Mizigo(tani) | Jumla ya ndege |
---|---|---|---|---|
2003 | 3.362.464 | -% | 51.826 | 62.439 |
2004 | 3.576.189 | 6. | 89.496 | 67.208 |
mwaka wa(2005). | 3.817.338 | 6.3% | 63.807 | 70.893 |
2006 | 3.848.757 | 0,8% | 83.598 | 74.650 |
2007 | 4,162,424 [2] | 7.5% | ||
2008 | 5,136,697 [2] | 23.5% |
Ndege na Sehemu za Usafiri
[hariri | hariri chanzo]Taminali 1 (Kimataifa)
[hariri | hariri chanzo]Makampuni ya ndege | Vifiko |
---|---|
Aero Contractors | Accra |
Afriqiyah Airways | Cotonou, Tripoli |
Air France | Paris-Charles de Gaulle |
Air Ivoire | Abidjan, Douala |
Alitalia | Rome-Fiumicino |
Arik Air | Accra, Banjul, Cotonou, Dakar, Freetown, Johannesburg, London-Heathrow, New York-JFK |
British Airways | London-Heathrow |
China Southern Airlines | Beijing-Capital, Dubai |
Delta Air Lines | Atlanta |
EgyptAir | Cairo |
Emirates | Dubai |
Ethiopian Airlines | Accra, Addis Ababa |
Iberia Airlines | Madrid |
Kenya Airways | Nairobi |
KLM | Amsterdam |
Lufthansa | Frankfurt |
Middle East Airlines | Beirut |
Nigerian Eagle Airlines | Abidjan, Accra, Banjul, Cotonou, Dakar, Douala, Libreville, Monrovia |
Qatar Airways | Doha |
Royal Air Maroc | Casablanca |
South African Airways | Johannesburg |
Turkish Airlines | Istanbul-Atatürk |
United Airlines | Washington-Dulles [begins 3 Mei][3] |
Virgin Atlantic | London-Heathrow |
Taminali 2 (Ndani au Taifa ukipenda)
[hariri | hariri chanzo]Makampuni ya ndege | Vifiko |
---|---|
Aero Contractors | Abuja, Benin City, Calabar, Enugu, Jos, Kaduna, Owerri, Port Harcourt, Warri |
Chanchangi Airlines | Abuja, Kaduna, Owerri, Port Harcourt |
Dana Air | Abuja, Enugu, Kano, Port Harcourt |
IRS Airlines | Abuja, Kano, Maiduguri, Yola |
Nigerian Eagle Airlines | Abuja, Kano, Owerri, Port Harcourt, Sokoto |
General Aviation Taminali (Ndani)
[hariri | hariri chanzo]Makampuni ya ndege | Vifiko |
---|---|
Arik Air | Abuja, Akure, Benin City, Calabar, Enugu, Gombe, Ilorin, Jos, Kaduna, Kano, Maiduguri, Owerri, Port Harcourt, Sokoto, Uyo, Warri, Yola |
Associated Aviation | Benin City, Ibadan |
Overland Airways | Ibadan, Ilorin, Minna |
Ndege za mizigo
[hariri | hariri chanzo]Makampuni ya ndege | Vifiko |
---|---|
Air France Cargo | Ndjamena, Paris-Charles de Gaulle |
Allied Air | Ostend |
Avient Aviation | Abidjan, Bamako, Châlons-en-Champagne, Libreville, Malabo, Ouagadougou, Pointe-Noire, Port Harcourt, Sharjah |
Cargolux | Luxembourg |
Jade Cargo | Sharjah |
Star Airlines (Macedonia) | Skopje, Bishkek, Sharjah, Hong Kong |
Ajali na matukio
[hariri | hariri chanzo]- Tarehe 23 Novemba 1996, wateka nyara walililazimisha Ethiopia Airlines Flight 961, kutoka Mumbai na Addis Ababa likielekea Abidjan kupitia masimamo mengi (pamoja na Lagos), kupata ajali katika Bahari ya Hindi.
- Tarehe 30 Januari 2000, Kenya Airways Flight 431 lililotarajiwa kutoka Nairobi hadi Lagos tena hadi Abidjan, lakini badala yake ndege lilielekea Abidjan. Ndege hiyo ilitumbukia majini baada ya kuondoka Lagos.
- Tarehe 28 Novemba 2003, udhibiti wa Lagos ulikubali Hydro Air 501, ndege aina Boeing 747-200 kutoka Uwanja wa ndege wa Brussels kutua katika Runway 19R. Ndege hiyo iligonga jiwe, kisha ikaelekea upande wa kushoto na injini yake ya kwanza huku ikigusana na jiwe hilo hadi “nosewheel” ikatua kwenye mtaro. Ripoti ya Wizara ya Ndege ilihitimisha kuwa sababu ya ajali ya ndege ilikuwa kwamba ndege ilipewa kibali cha kutua katika Runway ambao ilifaa kuwa imefungwa.
- Tarehe 22 Oktoba 2005, Bellview Airlines Flight 210, ilifaa kutua mjini Abuja, ilipata ajali baada ya kuondoka, na kuwaua watu wote waliokuwa ndani.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedFAAN
- ↑ 2.0 2.1 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-15. Iliwekwa mnamo 2023-07-01.
- ↑ http://www.united.com/press/detail/0,7056,61241,00.html
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Murtala Muhammed Airport Archived 17 Juni 2020 at the Wayback Machine.
- Current weather for DNMM at NOAA/NWS
- Accident history for LOS at Aviation Safety Network