Nenda kwa yaliyomo

Usimulizi wa hadithi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Usimulizi wa hadithi unafafanuliwa kutokana na maneno mawili yaliyounganishwa kutoa maana mpya ya pamoja.

Maana ya usimulizi[hariri | hariri chanzo]

Usimulizi ni namna ya kuelezea mtu au watu jambo fulani ambalo limetokea katika muda uliopita au zamani sana.

Kutokana na fasili hiyo tunapata aina mbili za usimulizi: usimulizi wa hadithi na usimulizi wa habari/usimulizi wa maandishina usimulizi wa mdomo.

kila namna ya usimulizi hutegemea msimuliaji anavyoweza kuwasiliana na msikilizaji.Ikiwa msikilizaji na msimuliaji hawakukaribiana njia itakayotumika ni ile ya maandishi.kwa mfano unataka kumueleza mtu aliyembali kuhusu jambo/tukio fulani utalazimika kutumia njia ya barua.

Lakini kama unamsimulia mtu ambaye yupo karibu nawe, utatumia njia ya ana kwa ana.

Maana ya hadithi[hariri | hariri chanzo]

Hadithi ni maelezo ya moja kwa moja ambayo yanahusu visa vilivyorithishwa toka zamani sana. Visa hivyo vingi huwa vya kubuni.

Viumbe wanaosimuliwa katika hadithi hii wanaweza kuwa wanadamu, wanyama, ndege na viumbe wengineo kama Malaika, mizimu, mazimwi.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usimulizi wa hadithi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.