Mikosi
Mikosi | ||
---|---|---|
Studio album ya G.W.M | ||
Imetolewa | 2000 | |
Aina | Hip hop | |
Lebo | GMC | |
Mtayarishaji | Rajabu Marijani Bonny Luv |
Mikosi, ni jina la albamu ya kwanza kutoka kwa kundi zima la muziki wa hip hop la Temeke Dar es Salaam, Tanzania maarufu kama G.W.M. Albamu imetoka mwaka wa 2000 - ukiwa mwaka wa matoleo mengi ya albamu za hip hop ya Tanzania kutoka. Hamasa ya kutoa albamu na kufanya uzinduzi zama hizi ndiyo hasa zilitamba. G.W.M ni moja kati ya makundi yanayoheshimika katika miaka ya 1990.
Walikuwa kufahamika haraka nchini Tanzania kwa ujuvi wao wa utunzi wa mashairi ulioendana na wakati ule. Walianza kutamba mwaka 1995 baada ya kutoa wimbo wa "Cheza mbali na kasheshe". Albamu hii ilitakiwa itoke tangu miaka ya 1990, lakini mipango ya kusaini mkataba wake ilienda kombo na kuja kutoka mwaka wa 2000, mbele kidogo baada ya kuvuma kwa sana. KR baaaye akajiunga na kundi la muda mfupi la Wachuja Nafaka. Nyimbo za katika albamu zilitayarishwa na Bonny Luv na Rajabu Marijani.
Orodha ya nyimbo
[hariri | hariri chanzo]Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatika katika albamu hii na maelezo yake ya msingi.
Upande | Jina la wimbo | Maelezo |
---|---|---|
A1 | Yamenikuta | Wakiwa na II Proud |
A2 | Bwana Kidevu | Wakiwa na G. Solo na Mc Steav |
A3 | Mguu Nje | Wakiwa na Dolla Soul |
A4 | Kipe Kitu | Ilivuta hisia kwa watu wengi wakati ule |
A5 | Mguu Nje Instru. | Midundo mitupu |
B1 | Mikosi | Wakiwa na Dre'z |
B2 | Mwenye Nyumba | Wakiwa na Dre'z |
B3 | Machizi Wangu | Wakiwa na Sloughter |
B4 | Autro | |
B5 | Machizi Wangu Instru. | Midundo mitupu |
Kikosi kazi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Mikosi katika wavuti ya Discogs