Usajili Internet wa Kikanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Usajili Internet wa Kikanda (kifupi chake kwa Kiingereza ni RIR yaani: regional Internet registry) ni shirika la kusimamia ugawaji na usajili wa idadi ya namba za internet ndani ya kanda fulani ulimwengu. Miongoni mwa namba wanazoshughulikia ni pamoja na anwani za IP (zote IPv4 na IPv6) na mfumo wa namba za kujitegemea (kwa matumizi ya kupanga taratibu nzima za BGP, yaani, jinsi ya kugawa mifumo ya mitandao kwa mpangilio, mitandao ya simu, data electronikia (na vilevile Internet).

Orodha ya usajili wa internet kikanda[hariri | hariri chanzo]

Sasa kuna RIRs tano katika operesheni:

  • American Registry for Internet Numbers (ARIN) [1] kwa Amerika Kaskazini na sehemu za Karibi
  • RIPE Network Coordination Centre (RIPE NCC) [2] kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia ya Kati
  • Asien-Pacific Network Information Centre (APNIC) [3] kwa ajili ya Asia-Pasifiki
  • Latin American and Caribbean Internet Addresses Registry (LACNIC) [4] kwa Amerika ya Kusini na maeneo ya kanda ya Karibi
  • African Network Information Centre (AfriNIC) [5] kwa ajili ya Afrika

Uhusiano kati ya RIRs na IANA[hariri | hariri chanzo]

Mamla ya Usajili wa Namba za Internet (kwa Kiingereza: Internet Assigned Numbers Authority au IANA) inasimama kama mwakilishi wa idadi ya namba za Internet kwa RIRs, halafu, kwa kufuata sera za ugawaji wa namba katika kanda kwa wateja wao, ambao pia inawajumlisha watoa huduma ya Internet, yaani, "Internet service provider" - halafu wao hutoa huduma hiyo kwa masharika au watu binafsi. Kwa pamoja, RIRs nao hushirkiana na Number Resource Organization (NRO),[6] iliundwa kama bodi wakilishi kwa ajili ya kukusanya mapato yao, kumaliza shughuli za kimuungano, na kueneza shughuli zao kimataifa. NRO imeingia mkataba na ICANN kwa ajili ya kuanzisha "Address Supporting Organisation"(ASO), yaani, Shirika la Kusaidia Anwani za Mtandao[7] ambalo lenyewe linashughulikia sera ya kimataifa ya anwani za IP ikiwa ndani ya sehemu ya kazi za ICANN.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

5 Kikanda internet registreringsenhet
Nyingine
ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usajili Internet wa Kikanda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.