Umoja, Sudan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Unity, Sudan)
Jump to navigation Jump to search

Majiranukta kwenye ramani: 9°0′N 29°42′E / 9°N 29.7°E / 9; 29.7

Unity (Wahda)


Umoja (Kar. الوحدة al-wahda) ni moja ya majimbo ("wilayat") 10 ya Sudan Kusini. Lina ukubwa wa eneo la 22,122 km 2 na wakazi wanaokadiriwa kuwa 4,700,000 (2000). Bentiu ndio mji mkuu wa jimbo hili. Lina wilaya tisa na ni eneo la mafuta baadhi ya mashamba yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Wakati serikali ya kitaifa mjini Khartoum inatambua jina la Alwahda = Umoja, serikali mpya ya sehemu ya Sudan Kusini inatambua jimbo hili kama Nile ya juu ya Magharibi (Western Upper Nile). Kabla ya mpangilio wa kiutawala wa mwaka wa 1994, Umoja ilikuwa sehemu jimbo kubwa la Upper Nile.

Umoja inakaliwa na makabila mawili, ya Nuer (wengi) na Dinka (wachache). Kama majimbo mengine ya Sudan Kusini, jimbo la Umoja linajumuisha wilaya tisa: Mayom, Rubkona, Parieng, Leer, Guit, Koch, Abeimnom, Mayendit na Payinjiar.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Kilimo ndio shughuli ya kiuchumi ya msingi katika jimbo hili . Watu ni wafugaji wahamaji ambao hujihusisha na kilimo na ugygaji, hasa ng'ombe. Kilimo hufanywa wakati wa msimu wa mvua ingawa baadhi ya ukulima pia hufanywa wakati wa majira ya joto. Mboga hazilimwi sana kwani wakulima wengi huishi vijijini kuliko mijini, na hivyo kukosa kupata masoko kwa mazao yao. Baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inawahamasisha wakulima kuanzisha utaratibu wa kilimo kwa ajili ya soko.

Uwanja wa Mafuta wa Unity[hariri | hariri chanzo]

Mafuta ya petroli ya kwanza ya Sudan iligunduliwa Umoja mwaka wa 1970. Makampuni ya mafuta ya kimataifa ambazo zinahusika katika kupeleleza mafuta katika Umoja zilichangia pakubwa kupoteza makaazi ya wakazi wazawa. [1]

Kiwanja cha mafuta cha Umoja kinapatikana ndani ya mgodi mkubwa wenye madini aina ya hydrocarbon katika bonde la ufa la Muglad na kina kadiriwa kuwa na mapipa milioni 150 ya mafuta. [2] Bomba Kubwa la Mafuta la Nile huanzia katika kiwanja cha mafuta cha Unity.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Human Rights Watch , 'Sudan, oil, and human rights', www.hrw.org , Novemba.
  2. NPA Group 2008, 'Sudan - Muglad Basin', www.npagroup.co.uk , 27 Februari. Retrieved on 5 Machi 2008.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]