Unguja Ukuu
Mandhari
Unguja Ukuu ni eneo la kiakolojia kwenye kisiwa cha Unguja, takriban kilomita 25 kusini-mashariki mwa Jiji la Zanzibar, ndani ya kata ya Unguja Ukuu Kaepwani. Utafiti wa wanaakiolojia (Chittick 1966; Juma 2004) ulionyesha kwamba huko kulikuwa na kituo cha biashara ya kimataifa mnamo mwaka 800 BK.
Kati ya mabaki yaliyogunduliwa kuna vyungu kutoka Ghuba ya Uajemi, pamoja na vipande vya vyungu vya China na vilulu kutoka Sri Lanka[1]. Kuna pia mabaki ya jengo la mawe kutoka enzi ya mnamo mwaka 900 linaloaminiwa kuwa msikiti[2].