Umakanika kwanta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Max Planck anahesabika kuwa baba wa nadharia ya kwanta.

Umakanika kwanta (kwa Kiingereza: Quantum mechanics; kifupi: QM) ni sehemu ya fizikia inayoeleza jinsi vitu vinavyounda atomi na mawimbi ya sumakuumeme (kama vile nuru) vinavyofanya kazi.

Hivyo umakanika kwanta huchunguza vitu tusivyoviona, kwa mfano kutokana na udogo wake, au vinavyosogea kasi mno, tofauti na vile vinavyochunguzwa na umakanika kawaida, sehemu ya kwanza ya umakanika.

Kwanta katika fizikia ni kiwango cha chini kabisa cha kipimo chochote cha kiumbo kinachohusika katika maingiliano.

Nadharia inayoelezea kwanta katika fizikia inaitwa nadharia ya kwanta na inazungumza kwamba vipimo vyovyote vya kiumbo vyawezavyo kupimwa hadi kiwango cha chini kabisa cha kwanta, kwa mfano: kiwango cha chini kabisa cha mwanga ni ukubwa wa fotoni, na kiwango cha chini kabisa cha chaji ni chaji ya elektroni.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Maelezo rahisi kidogo:

Maelezo ya kitaalamu zaidi:

     .

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

On Wikibooks

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Vitini
FAQs
Media
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umakanika kwanta kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.